Home LOCAL WAZIRI UMMY AKUTANA NA KAMATI TENDAJI YA CHAMA CHA WAUGUZI TANZANIA (TANA)

WAZIRI UMMY AKUTANA NA KAMATI TENDAJI YA CHAMA CHA WAUGUZI TANZANIA (TANA)

Waziri Afya Ummy Mwalimu katika kuendelea na utaratibu wa kukutana na vyama vya kitaaluma nchini, leo Agost 18, 2022 amekutana na kamati tendaji ya Chama cha Wauguzi Tanzania (TANA) kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaama.

Waziri Ummy amewashukuru na kuwapongeza Wauguzi wote nchini kwa kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha, Waziri Ummy alisema Wizara inatambua kazi kubwa inayofanywa na Wauguzi nchini na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa Weledi,miiko,maadili pamoja na kuzingatia viapo vya taaluma yao ili kuendelea kuendeleza agenda ya ubora wa huduma nchini.

Naye Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel amesema suala la afya ni usalama wa nchi,hivyo Uuguzi ni eneo linalobeba kwa asilimia kubwa kwente sekta ya afya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here