Home SPORTS YANGA MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO

YANGA MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO

Na: Mwandishi wetu.

MABINGWA wa kihistori Yanga  leo wameibuka kidedea katika fainali ya michuano Azam Federation  kwa mikwaju mikwaju ya penati 4-1 mchezo uliopigwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha.

Ilikuwa ni fainali moja yenye ushindani mkubwa ndani ya dk 120 ambapo ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ulikuwa unasoma Yanga 3-3 Coastal Union.

Ni mabao ya Abdul Seleman,’Sopu’ yeye aliweza kufunga yote matatu kwa Coastal Union huku kwa Yanga ni Feisal Salum,Heritier Makambo na Dennis Nkane hawa walifunga mabao kwa Yanga.

Ushindi wao Yanga leo ni wa penalti 4-1 ambapo kwa Coastal Union ni Victor Akpan pekee aliweza kufunga penalti hiyo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here