Ni ubunifu wa hali ya juu kutoka kwa mwalimu wa Ujasiriamali katika Chuo cha VETA- Karagwe mkoani Kagera Hamisi Jumanne katika kutengeneza kinywaji aina ya ‘Wine’ unatokana na tangawizi, Mchaichai na Amdalasini ambayo ni tofauti kabisa na aina nyingine za Wine zinazotengenezwa ndani na nje ya Tanzania.
Mwalimu Hamisi ameleta kinywaji hicho kwenye Maonesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya MwalimuJulius Nyerere Jijini Dar es Salaam yenye kauli mbiu isemayo Tanzania ni mahali sahihi kwa uwekezaji na biashara.
VETA wapo kwenye Maonesho hayo, kama kawaida yao wamekuwa wakileta Teknolojia ya vitu mbalimbali na kuvutia mamia ya watu wanaotembelea maonesho hayo ambapo mwaka huu 2022 wameongeza Bidhaa nyingi mpya zilizobuniwa na watanzania wenyewe kutoka katika vyuo vyao mbalimbali vilivyosambaa nchi nzima.
Moja ya Bidhaa mpya kabisa maonesho ya mwaka huu ni kinywaji cha Wine iliyotengenezwa kwa mchanganyiko maalum wa tangawizi, Mchaichai na Amdalasini kutoaka kwa Mwalimu wa Ujasiriamali Hamisi Jumanne ambapo hapa anaelezea ubunifu huo.
“Sisi VETA Karagwe tumekuja na kitu cha ubunifu kabisa na cha kipekee utengenezaji wa Wine kwa kutumia Mchaichai ,Amdalasini, Rozela pamoja na Tangazi ,huu ni utofauti mkubwa sana na ubunifu wa kipee ambao pia tumekuwa tukiwafundisha wanafunzi wetu kuona thamani ya vituo vingine.
“Wamezoea Mchaichai na Amdalasini unatumika kwenye chai tu lakini leo kwa ubunifu wetu uko kwenye Wine , ukiweka Wine kwa namna hii wanafunzi wakienda mtaani wataamua kujitegea wenyewe kwasababu watakuwa wamepata maarifa haya lakini itaongeza thamani na uchumi kwa wananchi.
“Ule Mchaichai na tangawizi vitalimwa kwa wingi sana ili waweze kuleta viwandani na viwandani vingine vinaweza kukua, kumbuka wanafunzi hawa ndio watakuwa wakurugenzi wa baadae.Kwa hiyo Wine hii ni tofauti na Wine nyingine kwani tuna fahamu zipo Wine zinazotengenezwa na Zabibu na Rozela lakini VETA Karagwe tumekua na Wine inayotokana na tangawizi, mchaichai na amdalasini.”
Amesisitiza hivyo Wine hiyo ni ya upekee kabisa unayoipata wilayani Karagwe Kagera na inafahamika kwa jina la Kombucha na mchanganyiko wake pamoja na mambo mengine umekuwa unasaidia kusafisha na kuimarisha mishipa, hivyo hata kwenye suala la tendo la ndio linakuwa liko vizuri lakini hairuhusiwi kwa walio na umri chini ya miaka 18.
Amefafanua kwa anayetaka Wine hiyo kwa sasa wako Sabasaba na wanaohitaji wanakaribishwa banda la VETA.“Lakini unaweza kupiga simu 0759 817029 ina maana ukiwasiliana na sisii basi tunakuletea popote ulipo kwani Serikali yetu imerahisisha masuala ya usafiri.
“Sisi kutoka Karagwe basi ikitoka kule asubuhi saa nane usiku inakuwa imefika Dar es Salaam na Wine itakuwa imekufikia.Watu wanavutiwa sana kwani kila ambaye ananunua anarudi tena kutokana na ule uasili uliomo kwenye Wine yetu.”
Watanzania na wananchi wote kwa ujumla mnapotembelea Maonesho ya sabasaba usiache kufika katika banda la VETA ukajionee bidhaa nyingi tofauti tofauti kutoka kwa wabunifu wetu wazawa ikiwemo kinywaji hiki cha Wine ya tangawizi, Mchaichai na Amdalasini.
Mwisho.