Home LOCAL WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MAONESHO YA 17 YA ELIMU YA JUU SAYANSI...

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MAONESHO YA 17 YA ELIMU YA JUU SAYANSI NA TEKNOLOJIA JIJINI DAR

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Watendaji wa Wizara ya Elimu na Tume ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU), baada ya kufungua Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Julai 19, 2022. Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Charles Kihampa, Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Penina Muhando na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Profesa James Mdoe.



Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa kwanza kushoto) katika Banda la Tume hiyo ambapo Mhe. Waziri Mkuu ametembelea kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na Tume hiyo.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi na Maofisa wa TCU katika Banda lao. PICHA NA: HUGHES DUGILO

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Sekta ya elimu ya Juu ni muhimili mkubwa katika kuleta chachu ya maendendeleo na kutoa mchango mkubwa wa kimaendeleo na ubunifu wa wataalamu mbalimbali hapa nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo Julai 19,2022 alipokuwa akifungua rasmi maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia aliyoyafungua rasmi  katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Sekta ya elimu ya Juu imekuwa na mchango mkubwa katika kusukuma gurudumu la maondeleo kwa kuhakikisha Taasisi zilizopo katika Sekta hiyo inazalisha wataalamu wa fani mbalimbali watakaoingia kwenye ushindani wa soko la ajira na kuleta tija katika Taifa.

“Sekta hii imekuwa na mchango mkubwa katika Taifa kutokana na kuzalisha wataalamu wa fani mbaimbali ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika soko la ajira na kuleta tija katika jamii” amesema Mhe. majaliwa.

Aidha amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi katika sekta ya elimu ya Juu  hususani kuongeza kiwango cha fedha kupitia Bodi ya mikopo ya elimu ya juu ili kila mtanzania mwenye sifa apate fursa hiyo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amepongeza ushiriki wa Sekta Binafsi kuwekeza katilka elimu ya juu ambapo mpaka sasa kuna vyuo Vikuu 28 na kwa kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais samia suluhu Hassan itaendelea kuiunga mkono Sekta Binafsi katika jitihada zake inazofanya ya kuwekeza katika elimu ya juu.

“Mchango wa Sekta Binafsi katika sekta nzima ya elimu hapa nchini ni mkubwa sana kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu, ni wazi kuwa Serikali imeendelea kutoa fursa kwa Sekta Binafsi kuwekeza katika  Sekta ya elimu na itaendelea kuthamini mchango wao” amesema Mhe. Majaliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TCU Prof. Penina Muhando amesema kuwa Maonesho hayo yanayofanyika kila mwaka yana lengo la kutoa fursa kwa Vyuo na Taasisi za elimu ya juu kukutana na wahitimu mbalimbali wa Kidato cha sita na wale waliomaliza vyuo vya kati ili wahitimu hao waweze kufanya uchaguzi wa kujiunga na Taasisi hizo pamoja na taasisi hizo kufahamiana.

Ameongeza kuwa TCU imeendelea kuratibu na kusimamia shughuli mbalimbali za Taasisi za elimu ya juu pamoja na kufanya uthibiti ili kuhakikisha zinatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu na ubora, pamoja na kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu wnapata fursa hiyo.

Maonesho ya Elimu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia ni maonesho yanayoratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu tanzania (TCU) yenye lengo la kutoa fursa kwa Vyuo hivyo kujitangaza na kuweza kukutana na wanafunzi sambamba na kufanya udahili wa Papo kwa hapo ambapo kwa mwaka huu Maonesho hayo yanafanyika katika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam ambapo yamefunguliwa rasmi leo Julai 17,2022 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. kassim Majaliwa Majaliwa.
Previous articleSHEREHE ZA UFUNGUZI WA MAONESHO YA 17 YA ELIMU YA JUU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Next articleBENKI YA TADB YALETA FURAHA KWA WAKULIMA NA VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA KANDA YA ZIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here