Home BUSINESS WATAALAMU KUTOKA NCHI ZINAZOZALISHA ALMASI AFRIKA ZASHUHUDIA MAFUNZO TGC

WATAALAMU KUTOKA NCHI ZINAZOZALISHA ALMASI AFRIKA ZASHUHUDIA MAFUNZO TGC

 

Wataalamu kutoka Nchi zinazozalisha Madini ya Almasi Afrika (ADPA) wamefurahishwa na mfumo wa mafunzo yanatolewa na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).

Wataalamu hao, wamekitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha baada ya kufika jijini humo kwa lengo la kuhudhuria Mkutano wa Tatu wa ADPA unaoanza tarehe 28 Julai.

Naye, Maurice Miema kutoka Jamhuri ya Kimokrasia ya Kongo amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika eneo la uongezaji thamani madini ambapo imeweza kuanzisha kituo cha mafunzo ya kuongeza thamani madini na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Aidha,  Miema amesema Tanzania ni nchi inayofaa kuigwa na nchi zingine za Afrika baada ya kuona uwekezaji mkubwa katika vifaa na mashine za ung’arishaji, ukataji na utambuzi wa madini ya vito.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) Daniel Kidesheni amesema timu ya wataalamu hao umefika kituoni hapo kwa lengo la kujifunza na kushuhudia shughuli za uongezaji thamani madini zinavyofanyika.

Kituo cha TGC ambacho kwa Afrika kipo Tanzania pekee kinatoa mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo ukataji na  ung’arishaji wa madini ya vito, utambuzi wa madini ya vito na usonara ambapo kwa sasa kuna zaidi ya wanafunzi 100 wanaosoma ngazi mbalimbali ikiwemo mafunzo ya muda mfupi na mafunzo ya muda mrefu.

Previous articleTANESCO SINGIDA YASAKA MAONI YA WANANCHI KUHUSU NISHATI YA UMEME
Next articleNAIBU WAZIRI MASANJA AKAGUA UJENZI WA NYUMBA MPYA 400 MSOMERA WILAYANI HANDENI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here