Home BUSINESS WAMKELE MENE KUFUNGUA MAONESHO YA 46 YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA

WAMKELE MENE KUFUNGUA MAONESHO YA 46 YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayotarajiwa kufunguliwa rasmi Julai 3,2022 Jijini Dar es Salaa. Waziri Kijaji alifanya ziara ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Biashara katika maonesho hayo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jumanne Sajini (Mb.) akizungumza naa waandishi wa Habari (hawamo pichani) mara baada ya kutembelea Mabanda ya wshiriki akiambatana na mwenyeji wake Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu kijaji (hayumo pichani katika Maonesho hayo.

KATIBU Mtendaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AFCFTA), Mheshimiwa Wamkele Mene anatarajiwa kufungua maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) Julai 03,2022 katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa leo Julai 02,2022 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashantu Kijaji alipotembelea katika viwanja vya maonesho hayo maarufu kama sabasaba yaliyoanza Juni 28, mwaka huu.

Waziri Kijaji amesema Septemba mwaka jana Bunge lilipitisha mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika na Januari mwaka huu ilipelekwa taarifa ya kuonesha utayari wa Tanzania kuingia katika eneo hilo la biashara.

“Kawaida wananchi walizoea maonesho yanazinduliwa na kiongozi wa nchi lakini mwaka huu itakuwa ni tofauti, Rais wetu Samia Suluhu Hassan alitoa fursa kwa sisi Watanzania kumkaribisha Katibu Mtendaji huyu na haya ni matokeo ya sisi kuingia huko katika mashirikiano,” Amesema Dkt. Kijaji.

Aidha Waziri Kijaji amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa maonesho hayo ambayo kwa kipindi hiki yameweza kuboreshwa kwa kiasi kikubwa na kuweza kuvutia wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

“Tujitokeze kwa wingi kuja kumsikiliza mgeni wetu rasmi ambaye atatuekeza fursa mbalimbali zilizopo katika soko hilo ili tuweze kuzitumia kwani tumerahisishiwa,” aliongeza.

Hata hivyo Waziri Kijaji amewataka wafanyabiashara kuanza kuzalisha bidhaa bora kwaajili ya soko la Afrika na sio Tanzania pekee ili kuweza kujitangaza kwa nchi mbalimbali na duniani kote.

“Tunakoelekea ni kwamba Afrika inataka kuwa soko huru ambapo biashara zitatoka nchi moja kwenda nyingine bila vikwazo vyovyote. Tulichokubaliana katika mkataba huo ni kwamba kila nchi iangalie sifa zipi za kipekee ambazo zikiweza kuchukuliwa na kutumiwa vizuri ndani ya Taifa hilo tunaweza kuzalisha kwa gharama nafuu na kuweza kuuza bidhaa zetu nje ya nchi.

“Na ndio maana mmeona wawekezaji wengi wanakuja nchini kwetu na hata Katibu Mtendaji huyu anakuja kuwaambia Watanzania Afrika tunakwenda kuwa soko moja, bidhaa zinazozalishwa Tanzania ziuzwe Afrika nzima,” Amesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here