Home LOCAL VITA YA MABADILIKO YA TABIA NCHI NI YA WOTE

VITA YA MABADILIKO YA TABIA NCHI NI YA WOTE

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Catherine Bamwenzaki.

Mkurugenzi wa JET, John Chikomo

Na:  Jimmy Kiango, MOROGORO.

WATANZANIA wametakiwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kulinda na kutunza mazingira.

Ieleweke kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi hazimkumbi mtu mmoja ama jamii fulani, badala yake yanaikumba nchi na wananchi wake bila kujali maeneo walipo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,Bi. Catherine Bamwenzaki.

Bi. Bamwenzaki aliyasema hayo wakati wa warsha ya siku moja iliyofanyika mkoani Morogoro ikiwahusisha wataalamu wa mazingira na Waandishi wa Habari za Mazingira nchini.

Lengo la warsha hiyo iliyoandaliwa na ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), lilikuwa ni kuwajengea uwezo na uelewa mpana waandishi wa Habari juu ya namna ya kushiriki katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo sasa yanaitesa dunia.

Akifungua warsha hiyo Bi. Bamwenzaki alisema wamedhamiria kukuza uelewa kwa wanahabari kuhusu mradi wa Taifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (NDC).

“Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kukabiliana na tatizo hilo, lakini kunahitajika nguvu ya pamoja katika vita hii, serikali peke yake haiwezi, ni vema ninyi wanahabari mkatumia kalamu zenu kuifahamisha jamii juu ya suala hili.

“Mabadiliko ya tabia nchi yana athari kubwa, miongoni mwake ni kuongezeka kwa joto, ukame, mafuriko na hata vimbunga, hivyo ni jukumu letu wote kushiriki katika kulinda mazingira,”alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), John Chikomo alisema anaamini warsha hiyo kwa wanahabari, itakuwa ni ufunguo wa kufungua uelewa wa jamii katika masuala yanayohusiana na changamoto hiyo.

“Twendeni tukaiambie jamii iachane na ukutaji miti, uchomaji mkaa na mambo mengine ambayo yanaharibu mazingira, twendeni tukawe mabalozi wa utunzaji wa mazingira,”alisema Chikomo.

MWISHO.

Previous articleMATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KISASA ZA UCHIMBAJI MADINI BARRICK YAVUTIA WANANCHI WENGI KATIKA MAONESHO YA SABA SABA
Next articleMAKINDA ASHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI ‘SANJO YA BUSIYA’ KUHAMASISHA SENSA KISHAPU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here