Home LOCAL TMDA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA...

TMDA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA KWENYE MAONESHO YA SABASABA


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo (kulia) akimsikiliza Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka hiyo Bi. Gaudensia Simwanza (kushoto) alipokuwa akifafanua jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mahojiano na waandishi wa habari kwenye maonesho ya sabasaba Julai 5,2022 Jijini Dar es es Salaam.

Na: Mwandishi wetu, DAR

MAMLAKA  ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),imewataka watanzania kuacha kutumia Dawa kiholela pale wanapojisikia kuumwa kutokana na madhara watakayoweza kuyapata kwa kukosa maelekezo sahihi kutoka kwa mtaalamu wa Afya baada ya kupata vipimo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Adam Fimbo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya Biashara ya  Kimataifa ya 46 ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Aidha Mkurugenzi huyo ameelezea umuhimu wa wananchi   alisema  ni muhimu kabla ya mtu kutumia dawa kufuata ushauri wa daktari.

“Utumiaji holela wa Dawa bila kufuata ushauri wa kitaalamu hupelekea madhara anayoweza kumpata mtumiaji kutokana na kukosa Maelekezo ya Daktari hii imekuwa changamoto katika jamii” amesema Fimbo.

Pia ameongeza kuwa Mamlaka hiyo inaendelea kufanya udhibiti wa Dawa Bandia kwa kuweka mfumo utakaowezesha kufanyika  ukaguzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo bandarini hadi katika masoko na kwamba kazi hiyo ni ya kila siku.

“Kazi yetu kubwa ni kuzikamata na matukio kama haya yapo na endapo tukibaini tunawakamata tunafanya ukaguzi kwa kushirikisha Jna jeshi la Polisi,”  ameongeza.

Katika hatua nyinge amezungumzia tatizo la kuzagaa kwa Dawa za kuongeza nguvu za kiume ambazo zimekuwa zikitumika kiholela na kuleta athari kwa watumiaji ambapo amesema kuwa Mamlaka hiyo imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na tatizo hilo sambamba na kutoa elimu kwa jamii ya watanzania na wananchi wote kwa ujumla juu ya madhara ya Dawa hizo.

“Kuna matukio mengi ya watu kupoteza maisha na wengine kupata shinikizo la damu kuzidi kuongezeka kwa kasi, hivyo tumeweka mkakati wa kuhakikisha tunatoa elimu kwa jamii nzima  kuacha kutumia Dawa hizi kiholela  kwa sababu zinasababisha vifo visivyotarajiwa na kuelimisha jamii matumizi sahihi ya kutumiaalisema.

MWISHO.

Previous articleBAKARI ATOA AJIRA KWA VIJANA KWA KUSAMBAZA GAS ORYX
Next articlePURA YAANDAA KAZIDATA MAALUM KUSAIDIA WATAALAMU SEKTA YA GESI, MAFUTA KUPATA AJIRA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here