Home SPORTS TIMU YA KIKAPU YA JWTZ YAREJEA NCHINI

TIMU YA KIKAPU YA JWTZ YAREJEA NCHINI

Na: mwandishi wetu

Timu ya Mpira wa Kikapu kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imerejea leo  Ikitokea nchini Ujerumani ilipokuwa inashiriki Mashindano ya Majeshi ya Dunia na kufanikiwa kushika nafasi ya Nne Kati ya Nchi 22 zilizoshiriki Mashindano hayo.

Akizungumza mara baada ya kuwasili Nchini Kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere, Kapteni Mohamed Kasui Mkuu Wa Msafara na timu meneja wa jeshi  Amesema anashukuru kwa matokeo chanya waliyoyapata katika Mashindano hayo ya Three On Three World Championship na wanaahidi kuendelea kufanya vizuri Kwenye Mashindano mengine.

Kwa Upande wake Shendu Mwangala Mwenyekiti wa chama cha kikapu Dar es salaam, Amesema Ushindi huo Umeweza kulitangaza Jeshi na Taifa kwa ujumla kupitia mchezo wa kikapu kwani sio jambo dogo kwa mara ya kwanza kuweza kufanya vizuri.

Timu hiyo iliondoka Nchini Tanzania Julai,03,2022 Kuelekea  Ujerumani katika mashindano  Ya kidunia Ya Three On Three World Championship iliyoshirikisha timu kutoka  mataifa mbalimbali Ikiwemo Marekani,Ufaransa,Saudi Arabia,Moroco.

Mwisho
Previous articleMETACHA KIPA MPYA SINGIDA BIG STARS
Next articleKAPAMA ATUA SIMBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here