Home BUSINESS STAMICO YAANZA RASMI KUUZA MKAA MBADALA WA MAKAA YA MAWE SABASABA

STAMICO YAANZA RASMI KUUZA MKAA MBADALA WA MAKAA YA MAWE SABASABA

Deus Magala Mkurugezi Rasilimali Watu shirika la Madini Tanzania STAMICO akizungumza na baadhi ya watu waliofika kwenye banda la hilo katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Ijumaa 1,2022 wa pili kutoka kulia ni Mhandisi Mchenjuaji Madini STAMICO Bi. Happy Manyange na kushoto ni Mhandisi Pili Athumani.

 Deus Magala Mkurugezi Rasilimali Watu shirika la Madini Tanzania STAMICO akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya watu waliofika kwenye banda la hilo katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam

Deus Magala Mkurugezi Rasilimali Watu shirika la Madini Tanzania STAMICO akizungumza na Mhandisi Pili Athumani katika banda hilo.

Wananchi mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Shirika la Madini Tanzania STAMICO katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

 Bw. Mwalogo afisa kitengo cha tehama Shirika la Madini Tanzania STAMICO akizungumza na Bi. Happy Manyange Mhandisi Mchenjuaji Madini STAMICO. PICHA NA JOHN BUKUKU

Na: Hughes Dugilo, DSM

Katika kuhakikisha Sera ya uhifadhi wa mazingira inatekelezwa kwavitendo Shirika la Madini la Taifa STAMICO limeanza rasmi kupeleka kwa wananchi Bidhaa yake ya mkaa mbadala na rafiki wa makaa ya mawe kwa ajili ya kuanza kutumika kwa matumizi ya nyumbni.

Akizungumza katika Mahojiano na waandishi wa Habari yaliyofanyika leo Julai 1,2022 katika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaa meneja Masoko na Uhusiano wa STAMICO Geofrey Meena amesema kuwa kwa sasa Bidhaa hiyo imeeanza kuuzwa na kwamba mpaka sasa tayari wameshapokea maombi mbalimbali ya mawakala kwaajili ya kusambaza bidhaa hiyo nchi nzima.

“Tumekuja hapa Sabasaba na Bidhaa yetu ya mkaa mbadala pamoja na mambo mengine, lakini tunataka kuwaeleza wananchi kwamba sasa bidhaa hii inapatikana hapa kweye maonesho, uzalishaji unafanyika katika kiwanda chetu kilichopo TIRDO Msasani na tunaenda kuandaa utaratibu wa kuwapata mawakala watakaosambaza mkaa huu nchi nzima” amesema Meena.

Na kuongeza kuwa “Mkaa huu ni mkombozi kwa wananchi kwani unweza kutumika kidogo kwa matumizi ya siku nzima na utasaidia sana kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na kukatwa misitu “ ameongeza.

Aidha amesema kuwa katika maonesho ya mwaka huu STAMICO wamekuwa na banda lao wao wenyewe ikishirikiana na baadhi ya Taasisi kutoka Sekta Binafsi zinazojihusisha na uchimbaji wa Dhahabu pamoja na kiwanda cha kusafisha Dhahabu kiichopo Jijini Mwanza.

Amezitaja Taasisi zilizoshirikiana na na STAMICO katika maonesho hayo ni pamoja na Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya Buckreef Mining Company, Buhemba Gold Mining na Kiwanda cha Mwanza Precious Metals refinery Limited cha Jijini Mwanza.

Kwa upande wake Mhandisi Mtaalamu Uchenjuaji Mandini kutoka STAMICO Happy Mbenyange anayesimamia Bidhaa hiyo amesema kuwa uzalishaji wa Bidhaa hiyo unakwenda vizuri ambapo kwa sasa mtambo wao una uwezo wa kuzalisha tani mbili kwa saa na kwamba wanatarajiwa kupokea mitambo mingine kwaajili ya kuongeza uzalishaji wa Bidhaa hiyo.

Pia amesisitiza kuwa Bidhaa hiyo ipo kwa wingi hivyo wananchi wanaweza kufika kwenye maonesho hayo kujipatia Bidhaa hiyo kwa bei nafuu.

“Mkaa upo wa kutosha na unapatikana hapa sabasaba wananchi wanaotembelea Maonesho haya wafike kwenye Banda letu la STAMICO kupata Bidhaa hii kwa bei nafuu” amesema happy.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here