Mgeni rasmi wa Bonanza la Maadhimisho ya Siku ya Timu ya Singida Veteran, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Ally Mwendo akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa bonanza hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Mulagiri lililofanyika leo Viwanja vya Peoples mjini hapa leo..
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Ally Mwendo akizungumza na washiriki wa bonanza hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Mulagiri lililofanyika leo Viwanja vya Peoples mjini hapa leo.
Katibu wa Timu ya Veteran Mkoa wa Singida , Gurisha Msemo akizungumza wakati wa uzinduzi wa bonanza hilo lililokwenda sanjari na maadhimisho ya kuanzishwa kwa timu hiyo.
Timu zikiwa uwanjani.
Wachezaji wakiwa uwanjani.
Bonanza likiendelea.
Timu picha ya pamoja.
Timu zikiwa Uwanjani.
Waamuzi wakiwakatika picha ya pamoja.
Mmenyano ukiendelea uwanjani.
Mtifuano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WACHEZAJI wa Timu ya Veteran Mkoa wa Singida wameadhimisha kuanzishwa kwa timu hiyo kwa kufanya bonanza la mchezo wa miguu na timu za maveteran kutoka mikoa ya Tabora na Dodoma mchezo uliofanyika Viwanja vya Peoples mjini hapa.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu wa Timu hiyo Gurisha Msemo alisema maadhimisho hayo yalikwenda sanjari na uhamasishaji wa zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika Agosti 23 mwaka huu nchini kote.
” Katika kuadhimisha siku hii moja ya kazi tulioifanya ni kuwatembelea watoto Yatima na wale waliotoka katika mazingira magumu wanaolelewa Kituo cha Upendo Hope kilichopo mjini hapa na kuwapa zawadi mbalimbali” alisema Msemo.
Mgeni rasmi wa bonanza hilo Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Ally Mwendo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Mulagiri aliwapongeza Veteran Singida kwa kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Mwendo alitaja baadhi ya faida za michezo kuwa ni afya, inajenga urafiki, undugu na ushirikiano pia ni ajira hivyo kila mtu anapaswa kuicheza.
“Lakini kama tunavyofahamu na kushauriwa na madaktari kuwa kunamagonjwa yasiyoyakuambukiza ambayo yanatoka kwa kufanya michezohivyo nawapeni hongera kwa kulijua jambo hilo” alisema Mwendo.
Aidha Mwendo alisema kama tunavyoona jinsi wanavyoshirikiana kati ya maveteran kutoka Tabora na Dodoma na kuwa huo ni mtandao uliotokana na michezo hivyo inapaswa kuendelezwa.
Mwendo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza kwa mara nyingine kwa kutumia maadhimisho hayo kuhamasisha sensa ya watu na makazi na kutoa faraja kwa Yatima jambo ambalo wamekwenda mbali zaidi tofauti na malengo ya kufanya bonanza pekee hivyo kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.
Pia Mwendo alisema kitendo cha kufanya maadhimisho hayo ni cha uungwana kwani wamejua umuhimu wake na kitafungua milango na kwa wengine hasa wanaochipukia katika michezo.
Aliwataka washiriki wa bonanza hilo kucheza kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote za michezo na washiriki mchezo huo kwa usalama pasipo kuumizana.