Home BUSINESS SERIKALI YA BRAZIL, WADAU KUWAONGEZEA NGUVU WAKULIMA WA PAMBA MWANZA

SERIKALI YA BRAZIL, WADAU KUWAONGEZEA NGUVU WAKULIMA WA PAMBA MWANZA

Na: Paul Zahoro, Mwanza RS

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ametoa rai kwa wadau wa Kilimo Mkoani Mwanza kuunga mkono jitihada zinazolenga kuboresha uzalishaji wa zao la pamba ili kuongeza kipato kwa wananchi kwani ndio zao kuu la biashara Mkoani humo.

Amesema hayo leo Julai 27, 2022 katika kikao kilichofanyika kwenye Hoteli ya Gold Crest mjini humo cha Kamati ya Uendeshaji Mradi wa zaidi ya Pamba ‘Beyond Cotton’ wenye thamani ya zaidi ya Tshs Bilioni 2 chini ya udhadhili wa Serikali ya Brazil na wadau wengine.

Mhe. Mkuu wa Mkoa amefafanua kuwa Miongoni mwa manufaa ya zao la Pamba ni kuwa linavumilia ukame ukilinganisha na mazao mengine hasa kwa kuzingatia mabadiriko ya tabia nchi ambapo mkoani humo wamekua wakikumbwa zaidi ya mabadiriko hayo.

Vilevile, Mkuu wa Mkoa ameishukuru Serikali ya Brazil kupitia ‘Brazilian Cooperating Agency’ kwa ufadhili wa Mradi huo nchini na ametoa rai kwa watumishi wa wizara ya Kilimo kuongeza ushirikiano kwenye mradi huo ambao utasaidia sana kufikia adhma ya serikali ya awamu ya sita ya kuinua kilimo ambacho ni nguzo kuu ya uchumi wa nchi.

Amefafanua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwainua wananchi wapatao takribani asilimia 65 waliojiajiri kwenye Kilimo na ndio maana imegawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani ambapo kwa Mwanza pekee wamepata Pikipiki 45 huku ikidhamiria kuwapatia maafisa Ugani wote 274 waliopo Mkoani humo.

Aidha, ametoa wito kwa wakulima kufuata maelekezo ya wataalamu wa Kilimo juu ya taratibu za kufuatwa kwenye kilimo cha pamba ili waweze kupata mazao mengi kama suala la upandaji wa kufuata sentimita 30 kwa 60 kati ya mche kwa mche na mstari kwa mstari ambayo husaidia kuongeza mazao.

Previous articleMAFUNDI UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA ILEMELA KUJENGA KWA NUSUBEI KUUNGA MKONO KAMPENI
Next articleTANESCO SINGIDA YASAKA MAONI YA WANANCHI KUHUSU NISHATI YA UMEME
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here