Home LOCAL RC SINGIDA : TATUENI KERO ZA WANANCHI MSISUBIRI HADI NIJE KWENYE ZIARA

RC SINGIDA : TATUENI KERO ZA WANANCHI MSISUBIRI HADI NIJE KWENYE ZIARA

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge  akizungumza na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri za wilaya na wakuu wa idara mbalimali leo Julai 6, 2022, wakati wa kikao maalum cha kufanya majumuisho ya ziara yake aliyoifanya hivi karibuni katika wilaya zote za mkoa huu kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya za Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao hicho kikiendelea.
Taswira ya kikao hicho.
Wakuu wa Idara mbalimbali za Serikali wa mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Wakuu wa Idara mbalimbali za Serikali wa mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya za Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.

Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na watendaji katika wilaya zote za mkoa huu kufanya ziara kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi badala ya kusubiri viongozi wa serikali ya mkoa ndio wazitatue changamoto za wananchi.

Ametoa agizo hilo wakati wa kikao maalum cha kufanya majumuisho ya ziara yake aliyoifanya hivi karibuni katika wilaya zote za mkoa huu kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Dk.Mahenge alisema serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo lakini wananchi hawajui kinachoendelea kwasababu viongozi ambao wanapaswa kuwaeleza hawafanyi hivyo.

“Ni muhimu mno kufanya mikutano ya wananchi kusikiliza kero zao, wahamasisheni madiwani, makatibu tarafa wafanye ziara, mkoa wetu mwaka wa fedha uliopita tulipata Sh.230 bilioni ni wajibu wetu kama viongozi kuzisimamia ili zilete tija katika maendeleo,” alisema.

Dk.Mahenge alisema wakuu wa wilaya wanajitahidi sana kufanya ziara na kusikiliza kero za wananchi lakini changamoto ipo kwa watendaji wengine wa serikali ambao hawafanyi hivyo na hivyo kusababisha kuibuka kwa kero nyingi ambazo kama ziara zingekuwa zinafanyika hali hiyo isingejitokeza.

Aliongeza kuwa katika baadhi ya maeneo wananchi wamekuwa wakilalamika kutoshirikishwa kwenye mipango mbalimbali ya maendeleo hususani baadhi ya wenyeviti wa serikali za vijiji ambao ndio wamekuwa na tabia hiyo.

“Baadhi ya wenyeviti wa vijiji wamekuwa kama miungu watu hawatowi fursa ya kusikiliza wananchi, RAS (Katibu Tawala Mkoa) tufanye uchunguzi na tuchukue hatua kwa kuzingatia sheria na taratibu za serikali,” alisema Dk.Mahenge.

Aidha, Dk.Mahenge aliagiza wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na wataalam wa ardhi kufuatilia migogoro yote ya ardhi na kuipatia ufumbuzi na kuiweka kwenye ‘data base’.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa huo kuwa yote aliyoyaagiza atayafanyia kazi kwa kushirikiana na Watendaji wa Halmashauri za Mkoa.

Previous articleVETA KIPAWA YAONESHA UMAHILI WAKE KATIKA UFUNDI WA SIMU ZA MKONONI
Next articleWINE YA MCHAICHAI, TANGAWIZI NA MDALASINI YAVUTIA WENGI BANDA LA VETA SABASABA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here