Home BUSINESS RAIS MWINYI AKOSHWA NA WAJASIRIAMALI WA TWCC, WAAMSHA SHANGWE NA KUMUIMBIA MAONESHO...

RAIS MWINYI AKOSHWA NA WAJASIRIAMALI WA TWCC, WAAMSHA SHANGWE NA KUMUIMBIA MAONESHO YA SABASABA

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake Tanzania (TWCC) Mwajuma Hamza (katikati) akitoa utambulisho wa Bidhaa za wajasiriamali waliopo katika Banda la Taasisi hiyo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ally Mwinyi alipotembelea Banda lao kujionea Bidhaa mbalimbali za Wajasiriamali hao sambamba na kujionea namna Cahama hicho kinavyotekeleza Majukumu yake Katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Mwenyekiti wa TWCC Taifa Mercy Silla.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ally Mwinyi (wa pili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa (TWCC) Mwajuma Hamza (wa pili kushoto) alipopita kwenye Banda lao kufanya ziara ya kuona Bidhaa za Wajasiriamali hao. (kulia) ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji, na (kushoto) ni Mwenyekiti wa TWCC Mercy Silla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ally Mwinyi akimsikiliza huku akipokea kadi kutoka kwa Mwenyekiti wa TWCC Mercy Silla mara baada ya kumaliza kutembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya Sabasaba Julai 4,2022 Jijini Dar es Salaam

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ally Mwinyi (kulia) akiagana na Viongozi wa TWCC mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea banda la Taasisi hiyo Kwenye Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. PICHA NA: HUGHES DUGILO.

DAR ES SALAAM.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindi Dkt. Husein Ally Mwinyi ameupongeza uongozi wa Chama cha Wanawake Tanzania (TWCC) kwa hatua kubwa waliopiga kwa jitihada kubwa wanazofanya katika kuwasaidia wanawake wafanyabiashara hapa nchini.

Rais Mwinyi ametoa pongezi hizo Julai 3,2022 alipofanya ziara katika Banda la Taasisi hiyo kujionea bidhaa mbalimbali za wajasiriamali waliopo chini ya TWCC katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kenye viwanja vya Mwalimu Juliua Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Rais Mwnyi alifika kwenye Maonesho hayo majira ya saa kumi za jionina kupokelewa na mwenyeji wake  Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TATRADE waandaji wa Maonesho hayo ambapo pamoja na mambo mengi alipata fursa ya kufanya ziara fupi ya kutembelea Mabanda mbalimbali na kujionea kazi mbalimbali za wafanyabiasha.

Akiwa TWCC Rais Mwinyi alipokewa kwa shangwe na sauti zikisikika za wajasiriamali hao kuimba wimbo wa ‘Baba Baba’  ikiwa ni ishara ya kumkaribisha huku Mwenyekiti wa TWCC Taifa na kurugezi Mtendaji wa Taasisi hiyo Mwajuma hamza wakimpitisha kwa wajasiriamali kuona kazi zao  huku wajasiriamali hao wakiendelea kumimba na kumpigia makofi.

Kwa upande wake Mweyekiti wa TWCC Mercy Silla amemshukuru Rais Mwinyi kwa kuwatembelea na kwamba ujio wake umeamsha hari kwa wajasiriamali wao na kufarijika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here