Home BUSINESS PROF: KAHYARARA: BIASHARA YA TANZANIA NA KENYA YAONGEZEKA

PROF: KAHYARARA: BIASHARA YA TANZANIA NA KENYA YAONGEZEKA

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema biashara kati ya Tanzania na Kenya imekuwa zaidi baada ya  ya makubaliano kati ya Tanzania na Kenya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru 49 kati ya 64  wakati vikwazo vingine 15 vilivyobaki vinafanyiwa kazi. 

Prof. Kahyarara ameyasema hayo Julai 6, 2022 wakati wa kipindi cha Morning Trumpet kinachoendeshwa na Kituo cha Televisheni cha Azam, jijini Dar es salaam

Amesema  katika kipindi cha mwaka mmoja (1) na miezi mitatu (3) cha Uongozi wa  Serikali ya Awamu ya Sita,   uwekezaji umeongezeka kutoka bilioni 1 hadi bilioni 9 na  Kituo cha uwekezaji kimesajili wawekezaji 380  wa ndani na nje ya nchi.

 Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza Mpango wa kuboresha mazingira ya biashara kwa kufuta tozo na kufanya marekebisho ya sera na sheria mbalimbali ili kuvutia wawekezaji na wafanyabiasha nchini na  kuongeza ajira, pato la taifa na kukuza  uchumi kwa ujumla. Amesema Prof. Kahyarara.

Akitolea mfano wa kongani ya viwanda ya Kwala iliyopo Kibaha inayotarajiwa kutoa ajira 100,000 za moja kwa moja na 500,000 zisizo za moja kwa moja, Prof. Kahyarara  amesema Serikali inalenga kuwa na viwanda vikubwa vingi vitakavyoanzishwa katika kongani za viwanda mbalimbali nchini kwa lengo la kuongeza ajira, pato la taifa na mauzo ya nje. 

Aidha, amesema Serikali imeanzisha  Mfumo wa Kielektroniki wa Huduma za pamoja kwa Wawekezaji unaounganisha taasisi 12 zinazohusika kuhudumia wawekezaji ili kupunguza urasimu na changamoto mbalimbali katika uwekezaji na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

Pamoja na Mfumo huo, Serikali pia imeanzisha Mfumo unaroa huduma za uhamiaji kwa mtandao hususan utoaji wa vibali vya Ukaazi (e-Permit) na Vibali vya kufanya kazi nchini kwa kuzingatia soko la ajira.

Katika kutatua changamoto ya  uhhaba wa mafuta ya kula, Prof Kahyarara pia amesema Serikali  inachukua hatua mbalimbali za kuongeza uzalishaji wa mazao yanayotoa mafuta ya kula pamoja na kuwawezesha wananchi kumiliki  viwanda vidogo na vya kati vya kuchakata mafuta hayo kupitia Programu maalumu ya Total Industrial Solution inayowawezesha wananchi kumili kiwanda ndani ya muda mfupi kwa gharama nafuu

Previous articleMTIBWA SUGAR YABAKI LIGI KUU
Next articlePROF: KAHYARARA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA KENYA YAONGEZEKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here