Home SPORTS MIKEL GUILLEN KOCHA MPYA WA VIUNGO AZAM FC

MIKEL GUILLEN KOCHA MPYA WA VIUNGO AZAM FC

 

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

KIKOSI cha Azam FC leo Julai 10 kimeweza kumtangaza kocha mpya wa viungo ambaye atakuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2022/23.

Anaitwa Mikel Guillen kutoka Hispania ambaye atakuwa ni kocha mpya wa viungo wa Klabu ya Azam FC.

Guillen ana uzoefu wa kufundisha timu za Aris Limassol ya Cyprus, inayoshiriki Ligi ya Conference European Cup, Bengaluru ya India na Dinamo Bucuresti ya Romania.

Uzoefu wake umemfanya kufundisha baadhi ya wachezaji wakubwa, akiwemo Sunil Chhetri, mfungaji namba sita wa mabao duniani kwa upande wa timu za Taifa.

Wengine aliowanoa ni Gordon Schildenfeld, aliyecheza fainali za Kombe la Dunia na Euro akiwa na Taifa lake la Croatia na Manu Garcia, aliyewahi kuwa nahodha wa Alaves kwa zaidi ya mechi 100 kwenye La Liga