Home LOCAL MHE. KABATI AONGOZA MAMIA YA WATU WENYE ULEMAVU KUPINGA UKATILI WA KIJINSI...

MHE. KABATI AONGOZA MAMIA YA WATU WENYE ULEMAVU KUPINGA UKATILI WA KIJINSI MKOANI IRINGA

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati akiwasalimu wageni waalikwa wakiwemo watu wenye ulemavu waliohudhuria Kongamano la watu wenye ulemavu wa Mkoa huo mara baada ya kupokea maandamano maalum ya watu wenye ulemavu yaliyoanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kupokelewa katika viwanja vya Garden vilivypo Posta katikati ya Mji wa Iringa leo Julai 9,2022 ambapo pamoja na mambo mengine lililenga kutoa Elimu ya Sensa kwa watu wenye ulemavu. 

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati akizungumza na watu wenyeulemavu na wageni wengine waalikwa alipokuwa akitoa hotuba yake juu ya Kongamano hilo na kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Iinga Queen Sendiga kuzungumza, 

Mkuu wa Mkoa wa Iinga Queen Sendiga akizungumza na hadhara iliyohudhuria katika Kongamano hilo alipokuwa akitoa hotuba yake kuzindua rasmi kongamano hilo lililofanyika leo Julai 9,2022 kwenye viwanja vya Posta katikati ya Mji wa Iringa. Mhe. Sendika ametumia jukwaa hilo kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia viivyokithiri katika mkoa huo na kuwataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu kutowaficha katika zoezi la Sensa linalotarajia kufanyika mwezi Ogasti, Mwaka huu.


Sehemu ya Umati wa watu wenye ulemavu wakisikiliza Hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi waliokuwa wakizungumza kwenye Kongamano hilo.

Mwalimu wa Shule ya Msingi visiwi Mkoa wa Iringa ambaye ni mtaalamu wa Lugha ya alama Mwl. Alikasuswe Mwandosya (kulia) akiwaongoza wanafunzi wake wenye ulemavu wa kusikia kutafasili hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na wageni waliopo meza kuu akiwemo Mgeni rasmi Mhe. Queen sendiga (hayumo pichani) kwenye Kongamano hilo lililofanyika Mkoani Irnga leo Julai 9,2022. PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO

Na: Hughes Dugilo, IRINGA.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati amewaongoza mamia ya watu wenye ulemavu wa Mkoa huo katika Kongamano maalum lililolenga kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kutoa elimu ya Sensa ili kuwajengea uelewa na kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika Mwezi Ogasti  Mwaka huu.

Kongamano hilo lililohudhuriwa na mamia ya watu wenye ulemavu kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Iringa lilianza kwa maandamano maalum yaliyoanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo na kupokelewa na Mgeni rasmi wa shughuli hiyo Mkuu wa Mkoa huo Queen Sendiga katika Viwanja vya Garden vilivyopo Posta katikati ya Mji wa Iringa.

Akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya utangulizi alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi, Mhe. Kabati amesema kuwa  imekuwa ni ndoto na kiu yake ya muda mrefu pia imetokana na kushuhudia changamoto nyingi wanazokumbana nazo watu wa makundi maalum hususani wenye ulemavu, wazee, watoto, yatima na  wanawake ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri a Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kupinga ukatili wa Kijinsia.

“Mhe Mgeni Rasmi kutokana na changamoto hizo nilianza kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha napunguza au kuondoa changamoto hizo kabisa”

“Baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kupeleka maswali na hoja zinazohusu watu wenye Ulemavu Bungeni ili kutafuta ufumbuzi ikiwemo mabadiliko ya kisheria na sera mbalimbali kuendana na mazingira yao”

“Hatua nyingine niliamua kuanzisha kampeni maalum ya kusaidia vifaa saidizi ikiwemo fimbo, basikeli, mafuta na hata kuboresha miundombinu katika baadhi ya maeneo ili wasikutane na changamoto hiyo” amesema Mhe. Kabati.

Aidha, ameongeza kuwa baada ya kuona hali ya uhitaji katika jamii ni kubwa, aliamua kuanzisha Taasisi maalum ya kushughulikia changamoto zinazowakabili  watu waliopo kwenye makundi maalum inayoitwa RITTA KABATI TRUST FUND, ambayo itajihusisha moja kwa moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto za watu wenye mahitaji maalum kwa kuwafuata kwenye maeneo yao na kuwatambua ili kufanya uratibu wa kuwasaidia.

“Taasisi hii inalenga Kukuza utu na heshima kwa watu wenye ulemavu na kutoa ushauri wa matibabu bila malipo kwa walemavu pamoaja na kusaidia miradi na shughuli nyingine za kiuchumi zinazoendeshwa na watu wenye ulemavu” ameongeza Mhe. Kabati.

Aidha amebainisha kuwa kazi nyingine ni kuanzisha na kudumisha vituo vya walemavu ili kusaidia jamii na kujihusisha katika michezo hususani ya watu wenye ulemavu kwa kuanzisha mashindano mbalimbali ya michezo na burudani katika Mkoa wa Iringa. 

Kazi nyingine ni pamoja na kusaidia programu na mipango inayolenga kuwaelimisha na kwafahamisha wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu kuhusu changamoto mahususi zinazowakabili watoto wenye ulemavu na jinsi ya kuwatunza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amempongeza Mbunge Kabati kwa hatua yake ya kusaidia watu wenye mahitaji maalum na kwamba kwa kufanya hivyo anaunga mkono jitihada za Serkali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vya ukatili hasa kwa watoto na walemavu.

Sendiga amsema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Mkoa huo unaongoza kwa ukatili wa kijinsia na kwamba jamii yote hususani wakazi wa Mkoa huo wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kutokomeza vitendo hivyo kama anavyofanya Mbunge Kabati.

“Ni aibu sana na fedheha kwa mkoa wetu kuongoza katika vitendo vya ukatili wa kijinsia, tunapaswa kupiga vita kwa nguvu zetu zote na mtu akikutwa na hatia ya kuhusishwa na vitendo hivi anapaswa kuchukuliwa hatua kali hata kufungwa maisha” amsema Mkuu wa Mkoa huyo huku akionesha kukasirishwa na vitendo hivyo.

katika hatua nyingine amezungumzia umuhimu wa watu wenye ulemavu kushiriki katika Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Ogasti mwaka huu na kuhimiza kuhesabiwa kwa watu wenye ulemavu na kwamba zoezi hilo  litaifanya Serikali kutambua idadi ya watu hao na hivyo kupata huduma kwa urahisi kutokana na mahitaji yao na maeneo walipo.

“Ndugu zangu naomba sana kuhamasisha wazazi na walezi kuhakikisha watu wote wenye ulemavu tulinao majumbani wanahesabiwa, usimfiche mtu mwenye ulemavu kwani kwa kufanya hivyo utaifanya Serikali kukosa idadi yao na hivyo kushindwa kuwafikia kuwapatia huduma zao wanazostahili” amesisitiza RC Sendinga. 

MATUKIO KATIKA PICHA MBALIMBALI ZA MAANDAMANO 

Previous articleMAWAZIRI WAIMWAGIA SIFA TPDC
Next articleKAYOMBO ATAMBULISHWA SIMBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here