Home BUSINESS MAWAZIRI WAIMWAGIA SIFA TPDC

MAWAZIRI WAIMWAGIA SIFA TPDC

Na Andrew Chale, Sabasaba.

MAWAZIRI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwemo Waziri wa Nishati Mh. January Makamba na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Ridhiwan Kikwete kwa nyakati tofauti wamelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuwezesha upatikanaji wa gesi hapa nchini.

Viongozi hao wamebainisha hayo kwa nyakati tofauti wakati walipotembelea ofisi za maonyesho TPDC ndani ya  Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Awali Waziri Makamba alisema TPDC ni miongoni mwa mashirika yenye tija hivyo Serikali itaendelea kuliwezesha na kuliwekea mikakati thabiti katika miradi yake.

Miradi hiyo ni pamoja na kuendelea ufuatiliaji wa gesi ikiwemo gesi asili na Nishati mbalimbali.

Katika hatua nyingine Mh. January Makamba alivutiwa na kasi ya uwekaji wa mfumo wa gesi katika magari hapa nchini kwani itaendelea kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia gesi hiyo inayopatikana hapa hapa nchini.

Kwa upande wake, Mh. Ridhiwan Kikwete alipongeza juhudi za TPDC katika kuendelea kujiimalisha upatikanaji wa gesi hapa nchini.

Aidha, Mh. Ridhiwan Kikwete alisistiza kwa Shirika hilo kuendelea kuongeza miundombinu zaidi ikiwemo vituo vya kutolea huduma.

“Nawapongeza kwa hatua mbalimbali katika masuala ya Nishati, muendelee kuimalisha vituo vya huduma.  Kule Chalinze jimboni kwangu mna kituo cha TAN-OIL, muendelee kuboresha zaidi na huduma ziwe kubwa” alisema Mh. Ridhiwan Kikwete.

Hadi sasa TPDC imebainisha kuwa, imegundua kiasi kikubwa cha gesi asilia futi za ujazo trilioni 57.54 ambapo mchakato wake ukikamilika wataweza kuimalisha soko la ndani na kuuza nje, Ambapo kiasi kikubwa cha gesi hiyo, kimegundurika baharini.

Aidha, gesi asilia imekuwa na matumizi makubwa ikiwemo  kuzalisha umeme ikichangia asilimia 62 kwenye gridi ya taifa.

Mwisho.

Previous articleMISA TANZANIA YAKUTANA NA WAHARIRI…KWAYU ATAKA MSUKUMO MABADILIKO YA SHERIA
Next articleMHE. KABATI AONGOZA MAMIA YA WATU WENYE ULEMAVU KUPINGA UKATILI WA KIJINSI MKOANI IRINGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here