Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa (aliyevaa suti) akizungumza kwenye mahojiano maalumu na kituo cha Utangazaji cha Azam TV mapema asubuhi leo julai 18,2022 katika viwanja vya mnazi mmoja ambapo Maonesho ya Vyuo Vikuu yanafanyika. Maonesho hayo yameanza leo na yatafunguliwa rasmi kesho Julai 19,2022 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Afisa Uthibiti Ubora wa TCU Esther Elia (wa pili kulia) akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika Banda lao kufahamu mambo mbalimbali yanayoendelea katika maonesho hayo na kupata elimu juu ya shughuli zinaofanywa na TCU katika Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yaliyoanza leo julai 18,2022 katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaa. (wa pili kushoto) ni Afisa Uthibiti wa TCU Bahati Dyegula.
Watumishi wa TCU Mwanaharusi Juma (wa kwanza kulia) na Joyce Lema (wa pili kulia) wakizungumza na wananchi waliofika katika Banda la TCU kupata maelekezo mbalimbali yakiwemo Udahili wa Papo kwa hapo unaofanywa naVyuo na Taasisi mbalimbali zinazoshiriki maonesho hayo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Afisa Uthibiti Mkuu wa Ubora kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Petro Mugandila (kushoto) akiwa na Afisa Mwandamizi wa Uthibiti Ubora wa Tume hiyo Aidan Mhonda (katikati) wakizungumza na kijana muhitimu wa kidato cha Sita aliyefika kwenye banda la Tume hiyo kupata maelezo mbalimbali kuhusu Udahili katika Viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam.
Muonekano wa Banda la TCU kwenye Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoratibiwa na Tume hiyo Jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO.