Home LOCAL KINANA:RAIS SAMIA MCHAPAKAZI MAKINI

KINANA:RAIS SAMIA MCHAPAKAZI MAKINI

*Huduma za jamii zimeimarika


 Na Mwandiahi wetu, Mbeya
Chama Cha Mapinduzi kimesema licha ya Rais samia suluhu  Hassan huzungumza  polepole lakini vitendo vyake katika utekelezaji wa sera za maendeleo zimekuwa motomoto.
Pia, serikali yake kwa muda mfupi imeaminika na kuheshimika kikanda na kimataifa.
Matamshi hayo yametamkwa jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana alipokuwa  katika Manispaa ya jiji la Mbeya.
Kinana alisema Rais Samia amekuwa kiongozi wa mfano ambaye kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja amekubalika katika medani za kidiplomasia huku akiaminiwa na taasisi za kimataifa.
Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025, alisema serikali yake imekuwa ikitekeleza  wajibu hatua kwa hatua na kuimarika kwa huduma za jamii.
“Rais Samia kiongozi mchapakazi asiye na majivuno. Kila uendapo utakutana na maendeleo ambayo hayakutegemewa yatokee  haraka. Anazungumza polepole lakini vitendo  ni vizito” Alisema Kinana.
Aidha, Makamu huyo Mwenyekiti alisema uongozi bora hupimaa kwa kutoa matokeo chanya ambayo kwa bahati nzuei kila sekta imepatiwa fedha  za kufanikisha miradi ya maendeleo.
“Kila eneo limegushwa katika maendeleo. Sekta za Maji,Afya ,elimu zimspatiwa fedha kusukuma mbele kwa muktadha wa kupunguza kero na  kumaliza changamoto sugu “Alisema Kinana
Hata hivyo kiongozi huyo aliwataka wanawake wengi zaidi kujitokeza katika kuwania nafasi za uongozi ili kukamilisha ndoto zao na kusema wanawake ni waaminifu na wasimamizi makini.

Previous articleKAMPUNI YA YARA TANZANIA YAWATOA HOFU WAKULIMA UPATIKANAJI WA MBOLEA MSIMU WA KILIMO
Next articleNIC YADHAMINI NA KUSHIRIKI KOROSHO MARATHON MTWARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here