Home SPORTS KAPAMA ATUA SIMBA

KAPAMA ATUA SIMBA

 

KLABU ya Simba leo imeingia makubaliano ya kumsajili kiungo Nyota Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.

Hata hivyo Kapama ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani kama beki, kiungo na mshambuliaji hali iliyolivutia benchi la ufundi na kumsajili.

Kabla ya kujiunga na Kagera  Kapama alikuwa akicheza Ndanda Fc,Kapama ni mzawa wa pili kutambulishwa ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuanza na Habib Kyombo ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Mbeya Kwanza.

Nyota huyu alikuwa anacheza Kagera Sugar msimu wa 2021/22 hivyo msimu wa 2022/22 atakuwa ndani ya kikosi cha Simba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here