Home SPORTS ILALA WAUNDA KIKOSI CHA WACHEZAJI 120 WA UMITASHUMTA DAR ES...

ILALA WAUNDA KIKOSI CHA WACHEZAJI 120 WA UMITASHUMTA DAR ES SALAAM

NA: HERI SHABAN (ILALA) herishaban@gmail.com

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam wameunda kikosi cha wachezaji 120 kwa ajili ya Mashindano ya Umoja wa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) Kanda ya Dar es Salaam.

Wachezaji hao 120 Wameweka kambi yao ya  siku kumi shule Kabby Academy iliyopo Ukonga Wilaya ya Ilala.

Akizungumza katika kufunga mashindano ya ngazi ya Wilaya llala Iliyoshirikisha Klasta nne za Halmashauri ya Jiji Kaimu Afisa Michezo Halmashauri hiyo ASHA MAPUNDA alisema wachezaji wote 120 wana afya nzuri leo wameanza kambi rasmi baada kumaliza michezo ngazi ya Wilaya ambapo katika timu zote tumechuja tumeweza kupata wachezaji wote 120  katika michezo mbalimbali watakuwa katika uangalizi Maalum.

“Timu yetu ya Halmashauri ya Jiji imejipanga vizuri kwa ajili ya kuchukua ubingwa tena mwaka huu tunaingiza wachezaji uwanjani tunatetea ubingwa wetu miaka minne yote Wilaya ya Ilala tumekuwa mabingwa na mwaka huu tunachukua kombe la Kanda ya Dar es Salaam” alisema Asha.

Asha alisema katika mashindano ya Kanda ya Dar es Salaam wanakutana na Wilaya ya Kinondoni,Temeke,Ubungo,na Kigamboni kutafuta timu moja itakayowakirisha Dar es Salaam mashindano ya ngazi ya Taifa yatakayofanyika Tabora mwaka huu.

Alisema katika wachezaji 120 wa Ilala waliounda leo baadhi yao  wachezaji wa soka la Wanawake na Wanaume, Netboli,kwaya,Ngoma, ,riadha 

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji,Abirah Nchia, alisema lengo kuu la mashindano hayo ngazi ya Wilaya kuibua vipaji vya michezo mbalimbali na kutambua wana michezo mahiri zikiwemo fani za ndani.

Previous articleMAKINDA ATINGA KWENYE MNADA WA OLD SHINYANGA AKIHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI SENSA
Next articleBENKI KUU YA TANZANIA KATIKA MAONESHO YA SABASABA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here