Home LOCAL HABARI PICHA; TAASISI YA USTAWI WA JAMII YASHIRIKI MAONESHO YA 17 YA...

HABARI PICHA; TAASISI YA USTAWI WA JAMII YASHIRIKI MAONESHO YA 17 YA VYUO VIKUU JIJINI DAR

Afisa Udahili wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Stanley Mbaga (kushoto mwenye fulana ya kijivu) akitoa melezo kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Taasisi hiyo kufamu shughuli mbalimbali za Kitaaluma zinazofanywa na Taasisi hiyo ikiwa pamoja na kufanya Udahili wa papo kwa hapo katika Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu yaliyanza leo Julai 18,2022 katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Mtumishi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Lulu Makata (kulia) akitoa maelezo kwa moja ya wahitimu wa Kidato cha Sita aliyefika kwenye Banda la Taasisi hiyo kwa lengo la kufanya usajili wa papo kwa hapo wa kujiunga na Chuo hicho katika mwaka wa Masomo wa 2022.

Afisa habari wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Benedict Nkwao (kushoto) akitoa elimu kwa mwananchi aliyefika katika Banda la Taasisi hiyo kupata maelezo na kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Vyuo Vikuu yaliyoanza rasmi leo kwenye viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Afisa Udahili wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Stanley Mbaga (kulia aliyekaa) akiwa na Mtumishi wa Taasisi hiyo Lulu Makata (wa pili kushoto) wakifanya udahili wa Papo kwa hapo kwa Mwanafunzi Rose Kishepo aliyefika kwenye Banda la Taasisi hiyo kwa lengo la kufanya usajili wa kujiunga na Chuo hicho. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here