Home BUSINESS FCC YATOA ELIMU YA BIDHAA BANDIA NA HALISI MAONESHO YA SABASABA JIJINI...

FCC YATOA ELIMU YA BIDHAA BANDIA NA HALISI MAONESHO YA SABASABA JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.William Erio akizungumza na waandishi wa habari katika Banda lao kwenye Maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa yaliyofunguliwa rasmi leo Julai 2,2022 kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.William Erio (kulia) akimsikiliza Naibu Waziri Exaud Kigahe (kushoto) alipokuwa akitembelea katika Banda la Taasisi kwenye maonsho ya sabasaba leo Julai 3,2022 Dar es Salaam.

Watumishi wa FCC wakifuatilia mahojiano ya waandishi wa habari (hawamo pichani) walipokuwa wakizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo William Erio (hayumo pichani) mara baada ya kumalizika kwa ziara fupi ya Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara aliyetembelea katika Banda hilo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. PICHA NA: HUGHES DUGILO.

DAR ES SALAAM.

Wito umetolewa kwa watanzania hususani wakazi wa Jijila Dar es Salaam na Viunga vyake kutemelea Banda la Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) katika Maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba yaliyoanza Juni 28,2022 na kufunguliwa rasmi leo Julai 3,2022 katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Wito huo umetolewa leo Julai 3.2022 na Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Taasisi hiyo na kusema kuwa ushiriki wao katika maonesho hayo kunatoa fursa kwa wananchi kuweza kupata elimu juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi.

Aidha amesema kuwa Taasisi hiyo inatekeleza jukumu la kumlinda Mtanzania kwa kuhakikisha wanasimamia vema Sheria zilizopo ili wananchi kupata Bidhaa zilizo na ubora na zilizokidhi viwango.

Pia Erio ameongeza kuwa Taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha mikataba kati ya walaji na watengenezaji pamoja na watoa inakidhi matakwa ya kisheria ili kutoa haki na kunufaisha pande zote.

“Hapa kwenye banda letu tutaonesha bidhaa mbalimbali bandia na bidhaa halisi, ili wananchi wapate kuzitofautisha, hivyo niwaombe wananchi watembelee na kupita  ili waweze kuzijua bidhaa hizo”. Amesema.

FCC wapo katika Banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambapo Taasisi zote za Wizrara hiyo zimeshiriki maonesho hayo.

Previous articleWAMKELE MENE KUFUNGUA MAONESHO YA SABASABA JULAI 3-2022 JIJINI DAR
Next articleMAKINDA ATINGA KWENYE MNADA WA OLD SHINYANGA AKIHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI SENSA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here