Home LOCAL CHUO KIKUU (MUST) CHAISHUKURU SERIKALI KWA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA KUJIFUNZIA NA KUFUNDISHIA

CHUO KIKUU (MUST) CHAISHUKURU SERIKALI KWA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA KUJIFUNZIA NA KUFUNDISHIA

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mawasiliano Chuo Kikuu cha Mbeya cha Sayansi na Teknolojia Dickson Msakazi (kushoto) akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari mwandamizi na Mkurugnzi wa Fullshangwe Blog, John Bukuku (kulia) katika mahojiano maalum na waandishi wa habari katika Maonesho ya 17 ya Vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Afisa Udahili wa Chuo Kikuu cha MUSTA loice Mambo (kushoto) akizungumza na wanafunzi waliohitimu kidato cha sita waliofika kwenye Banda la Chuo hicho kufanya udahili.

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha MUST Justine Mwakatobe akitoa maelezo kuhusu ndege isiyotumia rubani (DRONE) ambapo katika Chuo hicho wanafunzi wanafundishwa ubunifu wa kuzitengeneza.

Dkt. Fredrick Ojija (kulia) kutoka Idara ya Utafiti na machapisho Chuo Kikuu MUST akiwa na Afisa Udahili wa Chuo hicho Aloice Mambo (kushoto) wakiwa kwenye banda lao.

Muonekano wa banda la Chuo Kiuu cha Mbeya cha Sayansi na Teknolojia (MUST)

DAR ES SALAAM.

Chuo Kikuu cha Mbeya cha Sayansi na Teknolojia (MUST) kimeishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika Miundombinu mbalimbali ikiwemo majengo na zana za kujifunza na kufundishia kwa kutoa fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 40 kupitia  ufadhili wa Benki ya Dunia.

Akizungumza katika Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayofanyia katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam, kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo hicho Dickson Msakazi amesema kuwa fedha hizo zimekiwezesha Chuo hicho kujiimarisha katika maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu ya kitaaluma.

Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia fedha hizi ambazo zimefanikisha kufanya maboresho kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo vifaa vya kujifunzia, pale Chuoni tuna Maktaba kubwa ya kisasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi elfu 2500 kwa wakati mmoja yenye mifumo ya online, mwanafunzi anaweza kujisomea kupitia mtandao, hivyo halazimiki kushika kitabu”

“pia kwa sasa tuna maabara kubwa ya kisasa yenye uwezo mkubwa na inafanya uhandisi wa vifaa tiba, hivyo tunaishukuru sana Serikali” amesema Msakazi.

Amebainisha kuwa kwa sasa Chuo hicho kina wanafunzi elfu nane na kwamba kutokana na mpango wao wa miaka mitano Chuo hicho kitakuwa katika hatua nzuri zaidi na kuwa kati ya Vyuo Vikuu vikubwa hapa nchini na kuweza kudahili wanafunzi elfu tano.

Previous articleCHUO KIKUU MZUMBE CHATAMBULISHA PROGRAMU MPYA TANO ZA MASOMO MSIMU MPYA 2022/2023
Next articleUMUHIMU WA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA HABARI NA KUIMARIKA KWA UHURU WA KUJIELEZA TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here