Home BUSINESS CHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT) CHAPIGA KAMBI SABASABA, CHATOA HUDUMA YA...

CHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT) CHAPIGA KAMBI SABASABA, CHATOA HUDUMA YA CHAKULA NA KUFANYA USAJILI WA WANAFUNZI PAPO HAPO

Afisa Masoko na Mahusiano kwa Umma wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Eugin Malley (wa kwanza kulia) akizungumza na moja ya mwananchi aliyetembelea katika Banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Watumishi wa Chuo cha taifa cha Utalii Neema Urassa (wa kwanza kulia) na na Remmy Mgonyoro (wa pili kulia) wakizungumza na wageni waliofika kwenye banda lao kwa nia ya kupata elimu na kufahamu shughuli mbalimbali za Chuo hicho kwenye Maonesho hayo.


Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Afisa Masoko na Mahusiano ya Umma wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Eugin Malley  amaesema kuwa kwa sasa Chuo hicho kimepiga kambi katika Maonesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara ya sabasaba yanayoendela katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya shughuli na majukumu yake sambamba na kufanya usajili wa wanafunzi wapya wanaotaka kujiunga na Chuo hicho.

Akizungumza kwenye Mahojiano maalum katika Banda la Chuo hicho lililopo ndani ya Banda Kuu la Wizara ya Maliasili na Utalii, Afisa huyo amesema kuwa maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kufahamu shughuli zinazotekelezwa na chuo hicho kwa mujibu wa sheria.

Aidha amesema kuwa katika Maonesho hayo Chuo NCT kimeanzisha Dawati lausajili wa wanafunzi wapya wanaotaka kujiunga na Chuo hicho na kwamba wanapatiwa ushauri na maelekezo juu ya kozi mbalimbali zinazotolewa kwenye Matawi yote ya Chuo hicho yaliyopo Dar es Salaam, Arusha na Mwanza na kisha kufanyiwa usajili wa papo kwa hapo.

“katika Maonesho haya Chuo chetu kimeshhiriki kikamilifu kuonyesha shughuli mbalimbali tunazozifanya zikiwemo zile za Kitaaluma pamoja na kufanya usajili wa wanafunzi wapya hapa hapa” amesema Malley. Huku akitoa mwito kwa wananchi wote hususani wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Viunga vyake kufika katika banda la Chuo hicho.

Ameongeza kuwa katika maonesho ya Mwaka huu Chuo hicho kinatoa huduma ya Chakula na Vinjwaji kwa wananchi wote wanaotembelea maonesho hayo na kwamba huduma hiyo ni ya viwango kutokana nakwamba shughuli hiyo inasimamiwa na wataalamu wao kutoka katika Chuo hicho kwa kuwashirikiana na wanafunzi wanaopata mafunzo ya Huduma na Ukarimu katika Chuo chao.

“Kwenye Sabasaba tumekuja naHuduma ya Chakula hii ni sehemu ambayo wanafunzi wetu wanapata mafunzo kwa vitendo, vyakula vyetu hapa vimetengenezwa katika viwango vya hali ya juu hivyo tunawakaribisha wananchi wote kufika katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii na waatapata huduma nzuri ya chakula na vinywaji” Ameongeza.

Previous articleKUTANA NA NEEMA NGOWI MJASIRIAMALI ALIYEPIGA HATUA KATIKA BIDHAA ZA VIUNGO MAONESHO YA SABASABA
Next articleMATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KISASA ZA UCHIMBAJI MADINI BARRICK YAVUTIA WANANCHI WENGI KATIKA MAONESHO YA SABA SABA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here