Home BUSINESS BODI YA NAFAKA TANZANIA (CPB) YAAHIDI NEEMA KWA WAKULIMA

BODI YA NAFAKA TANZANIA (CPB) YAAHIDI NEEMA KWA WAKULIMA

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyika Tanzania (CPB), Dkt. Anselim Moshi akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam.

DAR ES SALAAM.

BODI ya Nafaka Tanzania (CPB) imesema dhamira yake  ni kuhakikisha mkulima mdogo anapata bei shindani katika mazao yake na inauwezo  mkubwa wa kuweza kununua mazao ya mkulima kwa bei shindani kwa kufanya uchambuzi na kujua mkulima anatumia gharama gani shambani.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, Mkurugenzi Mkuu,Dkt. Anselm Moshi amesema  bodi yao imekuwa ikihakikisha  mkulima anakuwa na masoko ya uhakika na kujenga  viwanda  kwa wingi.

Amesema wamekuwa wakijenga viwanda kila  mahali na  kuongeza kasi hiyo ili viwe soko ya mkulima katika kuuza mazao kwa urahisi.

Amesema ujenzi huo wa viwanda utaweza kutoa fursa kwa vijana kupata ajira na thaman  ya mazao yao  wanayozalisha yanaweza  kuuzwa katika masoko ya kimataifa na kuleta fedha katika nchi.

“Tukileta fedha nyingi katika nchi tutahakikisha mfumo wa bei unakuwa imara hauyumbiyumbi sana,”amesema na kuongeza. 

Amesema wakulima wengi kwa sasa wanamikataba mingi katika maeneo yao ambapo wapo 60,000 katika kilimo cha ngano ,alizeti ,maharage ya soya.

Aidha amesema tangu mwaka juzi wameanza mikakati ya kilimo cha mikataba kuhakikisha  kwamba wanafanya uhamasishaji wakulima waweze kulima na wizara ya kilimo kuhakikisha wakulima wanapata mbolea na pembejeo za wakati.

Amesema katika nchi kilimo cha ngano kilianguka na kukawa hawazalishi hivyo wakawa wanategemea kwa kiasi kikubwa kuagiza kutoka nje .”Tunaagiza sasa hivi ngano tan milioni 1 kila mwaka  ambazo tunatumia fedha za kitanzania Bilioni 530 kila mwaka …tunamaelekezo ya serikali ya kuhakikisha wanazalisha ngano ya kutosha Tanzania tufikie angalau tani Miliono 1 na zaidi ifikapo mwaka 2025.

“Tumeanza mwaka jana tumeanzisha mbegu kutoka Zambia tani 204 na kugawa kwa mkopo ile kanda ya kasikazini na matokeo yalikuwa mazuri,”amesema 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here