Home BUSINESS BENKI KUU YA TANZANIA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

BENKI KUU YA TANZANIA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo, akiweka saini katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina, akitoa maelezo kwa Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo (kulia) alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Idara ya Majanga BoT, Bi. Dorosela Blasius na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Bw. Augustino Hotay.


Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo, akifurahia jambo na Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi kutoka Bodi ya Bima ya Amana, Bi. Joyce Shala na Afisa wa Benki Bi. Rukia Muhaji katika banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Sabasaba.

Mhasibu Mkuu Mwandamizi BoT, Bw. Elirehema Msemembo, akielezea sarafu za BoT kwa watoto waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Bw. Augustino Hotay akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji BoT, Bw. Kened Nyoni, walipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma BoT, Bw. Lwaga Mwambande, akielezea namna ya kutambua Alama za Usalama za noti zetu kwa wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Shilole akitazama picha za noti za Benki Kuu ya Tanzania alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Beatrice Ollotu.

Mchambuzi wa Masuala ya Kifedha BoT, Bi. Laila Kisombe akitoa elimu kuhusu Uwekezaji katika Dhamana za Serikali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Previous articleILALA WAUNDA KIKOSI CHA WACHEZAJI 120 WA UMITASHUMTA DAR ES SALAAM
Next articleWMA YAANZISHA VITUO ZAIDI YA 5000 VYA UKAGUZI NCHI NZIMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here