Home BUSINESS BARRICK INATAMBULIWA KAMA MDAU MUHIMU KATIKA UKUZAJI WA UCHUMI WA KIJAMII TANZANIA

BARRICK INATAMBULIWA KAMA MDAU MUHIMU KATIKA UKUZAJI WA UCHUMI WA KIJAMII TANZANIA


Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, akikabidhi vocha ya dola za kimarekani 10,000 kwa Meneja Miradi ya Asasi isiyo ya Kiserikali ya Ikupa Trust Fund, Peter Charles, kwa ajili ya kusaidia miradi ya akina mama na watoto wenye ulemavu nchini baada ya kuongea na waandishi wa habari.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akikabidhi vocha ya dola za kimarekani 10,000 kwa Meneja Miradi ya Asasi isiyo ya Kiserikali ya ATFGM, Valerian Mgani na Sista Jaquline Bbaga, zilizotokana na jitihada zake za kufanikisha kukabili changamoto mbalimbali katika jamii.
Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow (kulia) kuhusu uwekezaji wa kampuni hiyo na jinsi inavyochangia kkuza uchumi wa kijamii nchini.Mkutano huo pia ulihudhuriwa na viongozi wa mkoa wa Mara na Wawakilishi wa Wananchi wa kata zilizopo jirani na Mgodi wa North Mara.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mark Bristow, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
Mbunge wa Tarime, Mwita Waitara akiongea wakati wa mkutano huo uliofanyika katika mgodi wa Barrick North Mara.
Baadhi ya viongozi wa vijiji vinavyo zunguka mgodi wa North Mara wakisiliza hotuba ya Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow( hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwekezaji wa kampuni na mchango wake katika kukuza uchumi wa kijamii wa Tanzania.

*
Kampuni ya Barrick Gold Corporation (NYSE:GOLD) (TSX:ABX) – Imetambulika kama mchangiaji mkubwa wa mapato ya Serikali katika mwaka 2021, na hivyo basi, kuthibitisha nafasi yake kama mchangiaji mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa kijamii Tanzania.

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu Mark Bristow, ameviambia vyombo vya habari hapa leo kuwa tangu kampuni ianze kuendesha migodi ya North Mara na Bulyanhulu mnamo mwezi Septemba 2019, jumla ya uwekezaji wake ni thamani ya Dola bilioni $1.995 za Kimarekani1. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, imelipa dola milioni $158 za Kimarekani kama kodi, mirabaha na ushuru; gawio kwa Serikali pamoja na mikopo ya uwekezaji yenye thamani ya dola milioni 42 za Kimarekani; na dola milioni 210 za Kimarekani kwa wazabuni wa ndani. Hadi hivi sasa, kampuni ya Barrick imekwishalipa dola milioni $140 kati ya dola milioni $300 za Kimarekani za maafikiano na Serikali.

“Tulipoingia ubia na serikali na kuanza kuiendesha migodi hii, ilikuwa ni mzigo mzito kwa Serikali na wawekezaji wao. Katika kipindi cha muda mfupi tulifanikiwa kuisuka upya, na kutengeneza kile ambacho kimsingi ni migodi miwili mipya. Migodi hiyo, hivi sasa, ipo katika nafasi nzuri ya kufikia uzalishaji wa kila mwaka unaotokana na miongozo iliyopewa na kampuni. Aidha, hivi sasa migodi ya North Mara na Bulyanhulu kwa pamoja inayo uwezo wa kufikia ngazi ya hadhi ya pamoja ya daraja la kwanza la uzalishaji (Tier 12 Complex). Hali hii ina inamaanisha kwamba migodi hii miwili kwa pamoja, inayo uwezo wa kufikia uzalishaji wa wakia angalau 500,000 za dhahabu kwa gharama zilizo chini ya wastani wa sekta ya uzalishaji wa dhahabu kwa kipindi cha zaidi ya miaka,” alisema Bristow.

“Tunaendelea kuchukua hatua endelevu kwenye maeneo tunayochimba madini na kuhifadhi mazingira katika migodi yote miwili na tunalenga fursa mpya pia. Katika hili, tumeendelea kujiimarisha katika maeneo ya Bulyanhulu kutokana na kupata leseni sita za kutafiti madini katika maeneo yanayopakana Jirani na mgodi huo. Aidha, tumewekeza katika kuboresha mifano (models) ya kijiolojia katika eneo la Kaskazini mwa Mkoa wa Mara na kubaini fursa katika sehemu nyinginezo za uwekezaji nchini Tanzania.”

Hali kadhalika katika kuhakikisha wazawa wanapewa kipaumbele shughuli za kampuni hiyo, na kwa mujibu wa sera ya Barrick ya ajira za ndani, wazawa wa Tanzania sasa wanachangia asilimia 96% ya nguvu kazi katika migodi yake miwili. Aidha, asilimia 64% ya wasimamizi wao wakuu wakiwa ni Watanzania. Migodi hiyo pia inayo dhamira ya dhati ya kuongeza ajira za Wanawake katika tasnia ya uchimbaji madini ambayo kwa muda mrefu imekuwa inaendeshwa na Wanaume kupitia mipango madhubuti inayolenga kuwaajiri na kuwaendeleza wafanyakazi hao.

Katika uwajibikaji kwa jamii, Barrick imetenga Dola 6 za Kimarekani kwa kila wakia moja ya dhahabu inayouzwa na migodi hiyo miwili kwa ajili ya kuboresha huduma za afya, elimu, miundombinu na upatikanaji wa maji safi ya kunywa katika jamii zinazoizunguka migodi hiyo.

Dola nyingine milioni 70 za Kimarekani zimetengwa kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya kitaifa ya inayolenga kuongeza thamani kwenye miradi mbalimbali ya kitaifa, inayojumuisha mafunzo yanayohusu madini na vifaa vya kisayansi katika vyuo vikuu vya Tanzania.

Katika nyanja ya usalama kazini, mgodi wa Bulyanhulu ulitangazwa kuwa mshindi wa jumla wa tuzo ya Tanzania ya OSHA (Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi) kwa mwaka 2022 huku ule wa North Mara ukitunukiwa tuzo ya mpango bora wa uhamasishaji wa afya ya jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here