Home BUSINESS APONGEZA JITIHADA ZA WIPO KUENDELEZA UBUNIFU

APONGEZA JITIHADA ZA WIPO KUENDELEZA UBUNIFU

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa amepongeza Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) kwa jitihada linazozifanya za kuendeleza kazi za ubunifu kwa maendeleo ya  nchi wanachama. 

Pongezi hizo amezitoa wakati akiwasilisha taarifa ya nchi  kuhusu  Miliki Ubunifu na ushirikiano  kati ya Tanzania na WIPO  katika Mkutano Mkuu wa 63 wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO), unaofanyika Geneva Uswisi.

Bw. Nyaisa  amesema  jitihada hizo  za kuendeleza kazi za ubunifu kwa maendeleo ya nchi wanachama, zitazaa matunda na kuendeleza bunifu mbambali na kuleta tija kwa nchi wanachama.

Ameeleza pia ushirikiano  kati ya Tanzania  na WIPO utalenga katika kusaidia wajasiriamali na vijana katika kutumia Miliki Ubunifu kwa maendeleo ya ubunifu.

Mkutano  huo wa siku saba ulioanza tarehe 14 Julai, 2022,  unahudhuriwa pia na  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Bishara na Mali,  (BPRA) Zanzibar, Bi. Mariam Mliwa Jecha, Mkuu wa Idara ya Uraghbishi wa Ushindani kutoka  Tume ya Ushindani (FCC) Bi. Magdalena  Utouh pamoja na Msajili Msaidizi Mkuu kutoka BRELA, Bi. Loy Mhando.

Previous articleONESHO KUBWA LA UTALII KUFANYIKA TANZANIA
Next articleWAZIRI BASHUNGWA ATOA MIEZI MITATU KITUO CHA AFYA KIBONA KIKAMILIKE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here