BAADA ya Kukaa Miaka minne bila taji la Ligi hatimaye Mabingwa wa Kihistoria Tanzania Bara Yanga wametwaa ubingwa wa 28 wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuichapa mabao 3-0 Coastal Union na kufikisha Pointi 67 ambazo haziwezi kufikiwa na watani zao Simba Mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
Yanga walipata bao dakika ya 34 likifungwa na Fiston Mayele likiwa bao lake la 15 hadi mapumziko wananchi walienda wakiwa wanaongoza kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko huku Yanga wakinufaika na mabadiliko hayo mnamo dakika ya 51 Chico Ushindi aliwanyanyua mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao la pili akimalizia pasi ya Fiston Mayele.
Mzee wa kutetema Mayele alirudi tena kambani katika dakika ya 67 aliifungia Yanga bao la tatu akimalizia pasi ya Fei Toto huku likiwa bao lake la 16 na kumuacha George Mpole akiwa na mabao yake 15.
Kwa ushindi huo Yanga wameivua rasmi ubingwa Simba yenye Pointi 51 ikiwa imecheza mechi 25 wakiwa na mechi tano mkononi ikumbukwe kuwa Yanga mapaka sasa hawajapoteza mechi yoyote ya Ligi Kuu Msimu huo na wakiwa wamebakiwa na mechi tatu Mkononi.
Mechi nyingine Azam FC wameishusha Geita Gold FC katika nafasi ya tatu baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya vibonde wa Ligi hiyo Mbeya Kwanza.