Home SPORTS YANGA YAKABIDHIWA RASMI KOMBE LA UBINGWA

YANGA YAKABIDHIWA RASMI KOMBE LA UBINGWA

   WACHEZAJI pamoja na Benchi la Ufundi la Yanga wakisherekea ubingwa wao mara baada ya kukabidhiwa rasmi kombe lao la ubingwa wa msimu wa 2021/22.

MABINGWA Wapya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara Yanga wamekabidhiwa Kombe la Ubingwa wa 28 baada ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City baada ya kutoshana nguvu ya kutoka sare ya bao 1-1 mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mshambuliaji  Heritier Makambo alianza kuifungia Yanga dakika ya 40, kabla ya kiungo Mganda, Joseph Ssemunju kuisawazishia Mbeya City kwa penalti dakika ya 50 kufuatia Nahodha, Bakari Mwamnyeto kuunawa mpira kwenye boksi.

Yanga wanafikisha mechi 29 bila kupoteza mechi, wakiwa tayari mabingwa kwa pointi zao 71, nyuma yao wakiwa mabingwa wa misimu minne iliyopita, Simba SC wenye pointi 60 za mechi 28 na kesho watamenyana na Tanzania Prisons hapo hapo Sokoine, Mbeya.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here