Home SPORTS WASHIDI MICHUANO YA TFS GOLF OPEN 2022 WAKABIDHIWA ZAWADI

WASHIDI MICHUANO YA TFS GOLF OPEN 2022 WAKABIDHIWA ZAWADI



Na: Stella Kessy

MCHEZAJI wa gofu wa Lugalo Isihaka Daudi ameibuka kidedea katika shindano la TFS Lugalo Open 2022 lililomalizika jana juni 19 jijini Dar es salaam.

Isahaka Daudi aliibuka kinara kwa kupiga mikwaju 75 siku ya kwanza na 70 siku ya pili na hivyo kupata jumla 145 akifuatiwa na Victor Joseph wa Dar Gymkhana wa pili kwa mikwaju 75 siku ya kwanza na 75 siku ya pili ikikamilisha jumla 150.

Katika mashindano hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili juni 18 na 19 Anold Kinyaiya mwanasheria na muwakilishu Ofisi ya Mkuu wa wilaya kinondoni ameipongeza klabu ya jeshi ya Lugalo kwa namna ambavyo imeendelea kukuza mchezo huo.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo Brig Jenerali Michael Luwongo Mstaafu amewapongeza wanahabari ambao wamekua wakiitangaza gofu kila mara huku akisema hamasa hiyo itumike katika kuuendeleza mchezo kimataifa.

Upande wa Makundi Divisheni A Mshindi wa kwanza ni Nicholous Chitanda mikwaju ya jumla 144 akifuatiwa na John Hiza mikwaju ya jumla 145 wote wa Lugalo.

Divisheni B mshindi wa kwanza ni Marcell Lubuva wa Lugalo aliyefungana na Michael Palangyo wa kili gofu Arusha kwa mikwaju 142.

Divisheni C mshindi ni Cyril Brown wa kili gofu mikwaju ya jumla 143 akifuatiwa na Nsajigwa Mwansasu wa Lugalo aliyechapa mikwaju ya jumla 145



Aidha upande wa wanawake mshindi ni Angel Eaton wa Lugalo mikwaju 82 siku ya kwanza na 77 siku ya pili ikikamilisha jumla 159 nafasi ya pili ikichukuliwa na Victoria Elias nae wa Lugalo mikwaju 82 siku ya kwanza na 80 siku ya pili jumla 162.

Mikwaju ya jumla kwa wanawake Mshindi wa kwanza ni Amina Nkungu 145 wa pili ni Loveness Frank wa Kili gofu 147 mikwaju 147.

Wachezaji waliopiga umbali mrefu mshindi wa upande wa wanaume ni Isihaka Daudi na wanawake ni Ayne Magombe wote wa Lugalo huku zawadi ya kupiga mpira karibu kabisa na shimo Wanaume ilichukuliwa na Elisha Fadhil na wanawake ni Angel Eaton.

wachezaji wazee wa wanaume mshindi wa kwanza ni Joseph Tairo mikwaju ya jumla 152 akifuatiwa na Julius Mbilinyi 157.

mwisho
.

Previous articleWAZIRI NNAUYE ASISITIZA MATUMIZI SALAMA YA TEHAMA KWA WANAFUNZI
Next articleWAZIRI AWAPONGEZA MABINTI KWA KUTWAA UBINGWA WA KRIKETI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here