Home BUSINESS WANAFUNZI CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WATAKIWA KUWA MABALOZI WA MILIKI UBUNIFU

WANAFUNZI CHUO CHA UFUNDI ARUSHA WATAKIWA KUWA MABALOZI WA MILIKI UBUNIFU

Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha, wametakiwa kuwa Mabalozi wazuri kwa vijana wenzao kwa kuhakikisha kuwa elimu ya Miliki Ubunifu inawafikia vijana wengi.

Afisa Mwandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni  (BRELA), Bw. Raphael Mtalima ametoa wito huo mapema leo tarehe 15 Juni, 2022 Jijini Arusha, wakati akitoa elimu ya Miliki Ubunifu chuoni hapo yenye lengo la   kuwajengea uwezo.

Bw. Mtalima ameeleza kuwa wanafunzi hao wanapaswa kuwa mawakala wazuri kwa kufikisha elimu ya Miliki Ubunifu katika jamii  inayowazunguka na mahali popote watakapokwenda .

Amesisitiza kuwa wakiielewa elimu hiyo inayotolewa na BRELA, itakuwa rahisi  kuisambaza kwa jamii kwa ujumla.  

Bw. Mtalima amesema  BRELA kwa sasa imejikita kutoa elimu ya Miliki Ubunifu katika Vyuo Vikuu na vya Kati lengo likiwa ni kuzalisha kizazi chenye uelewa mzuri wa Ubunifu.

“Vyuo vingi vya ufundi kazi zao nyingi ni za Ubunifu hivyo elimu hii itawahamasisha na kutambua umuhimu wa kurasimisha bunifu zenu mnazozivumbua,” amefafanua Bw. Mtalima.

Aidha Bw. Mtalima amesema kuwa utoaji wa elimu hiyo vyuoni  utawapatia vijana fursa ya kuzidi kuvumbua  kwani kwa sasa vijana wengi wamekuwa na weledi wa kutosha na chachu kubwa ya kujifunza.
 
Ameongeza kuwa baada ya kupata elimu hiyo wanatakiwa kuwasilisha  BRELA  vumbuzi zao kupitia mfumo wa Usajili kwa njia ya mtandao(ORS) unaopatikana katika   tovuti  ya BRELA, www.brela.go.tz

Previous articleMKUU WA MKOA WA RUVUMA AKABIDHI PIKIPIKI 286 KWA MAAFISA UGANI,AWATAKA KWENDA KUSIMAMIA NA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MASHAMBANI
Next articleYANGA YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA NBC 2O21/2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here