Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian kwenye uzinduzi wa soko la tumbaku kwa kampuni mpya kutoka mkoani Iringa ya ‘Mkwawa Leaf Tobacoo company Limited.
Mkurungezi wa kampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku ya Mkwawa Leaf Tobacoo company Limited Ahmed Mansour akitoa neneo wakati wa ufunguzi wa soko la Taumbaku miemba mkoani Tabora.
Baadhi ya wakulima kutoka vyama mbalimbali vya ushirika wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tabora .
Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi bodi ya Tumbaku Tanzania kulia ni mkurungezi mkuu wa bodi ya Tumbaku Tanzania Stanley Mnozy ,kushoto ni makamu mwenyekiti wa bodi hiyo Hassani Wakasuvi na wa pili kushoto ni mjumbe wa bodi Said Ntahondi .
Na: Lucas Raphael,Tabora
Wakulima wa mazao ya Tumbaku na Pamba mkoani Tabora watakaobainika kuweka uchafu kwenye mazao hayo watachululiwa hatua kali za sheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani. .
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian kwenye uzinduzi wa soko la tumbaku kwa kampuni mpya kutoka mkoani Iringa ya ‘Mkwawa Leaf Tobacoo company Limited’ iliyoanza ununuzi wa zao hilo uliofanyika katika magahala ya Miemba mkoani Tabora .
Alisema kwamba kampuni hiyo imekuja kufufua zao la tumbaku hivyo ni muhimu kwa wakulima kulima zao la Tumbaku iliyobora ili kuweza kupata bei nzuri na sio kuweka uchafu ambao utaharibu sifa ya mkoa huo.
Balozi Dkt Batilda kwamba mazao bora ndio yatawafanya wakulima kupata bei nzuri mazao yao ambayo miaka miwili soko hilo lilishindwa kufanyika kutokana na wakulima kulima kwa kuongopa na kushuka kwa bei ya zao hilo kuwaliwafanya wakulima kusita kulima Tumbaku.
“ndugu wakulima sintasita kuwafikisha mahakamani kwa kosa la kuchanganya uchafu ikiwemo mchanga majiani na tumba isyostahili kwenye tumbaku nzuri katika swala hili mtanisamehe ila mkitaka tuelewane wakulima pangeni vizuri tumbaku yenu na mtapata bei nzuri.” Balozi Dkt Batilda
Aidha mkuu wa mkoa aliwataka wakulima kuzalisha tumbaku kwa wingi na yenye ubora kwa msimu ujao wa kilimo, kwa kuwa tayari Serikali imeweka mazingira wezeshi ya kuwa na soko la uhakika
Awali mkurungezi mkuu wa bodi ya Tumbaku Tanzania Stanley Mnozy alimweleza mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda kwamba zao la tumbaku lilikabiliwa na changamoto kubwa ya baada ya kuondoka kwa kampuni ya TLTC sekta hiyo iliyumba na sasa kumejitokeza kampuni ya Mkwawa ambayo itanunua tumbaku mkoani hapa msimu huu .
“licha ya kuyumba kwa sekta hiyo sasa sekta hiyo itasaimama tena kwa wakulima kzao la Tumbaku kuunza na kulipwa fedha zao kwa wakati hivyo waklulima wasiwe na hofu “ alisema Mkurungezi Stanley Mnozy
Alisema kwamba wakulima za wazao la Tumbaku wamepata faraja kubwa kwa kujitokeza kwa mnunuzi mwingine mwenywe uwezo mkubwa wa kurudisha na kukuimarisha zao la Tumbaku nchini.
Hata hivyo mkurungezi wa kampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku ya Mkwawa Leaf Tobacoo company Limited Ahmed Mansour aliwahakikishia wakulima kwamba kampuni hiyo imejipanga kununua tumbaku ya kutosha.
Aliwakata wakulima wa zao la Tumbaku nchini kulima zao hilo liwe bora na lenye tija kwa wakulima nchi kwa ujumla.
“Tumekuja wazalendo wa nchi hii tumekuja wakuwakomboa wakulima za wao la Tumbaku ambao hawakulipwa fedha zao miaka miwili iliyopita na sasa kampuni ya Mkwawa Leaf itawalipa baada ya siku nne mara baada ya kununuliwa kwa Tumbaku hiyo”alisema Ahmed .
Hata hivyo aliwaeleza kwamba Kampuni ya Mkwawa inayonunua tumbaku mkwawa huu itawalipa wakulima kila kilo ya tumbaku itakayounzwa hataongeza shilingi 30 na kwa wale walikuwa wanadaiwa kila kilo hatalipa shilingi 50 kwenye deni la nyuma.
Kwa muda mrefu sasa wakulima wa zao la Tumbaku walikuwa na kilio cha kutokuwa na soko la uhakika jambo ambalo limekuwa likikwamisha jitihada zao katika kulima zao hilo
Zaidi ya tani 30 000 za tumbaku zinatarajiwa kununuliwa kwa mkoa wa Tabora huku mnunuzi mpya kampuni ya Mkwawa Leaf Tobacco co. ltd yeye amekusudia kununua zaidi ya kili milioni 10 kwa msimu huu
Mwisho