Home SPORTS WAKALA WA MISITU TANZANIA (TFS) KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA “MOI MARATHON”

WAKALA WA MISITU TANZANIA (TFS) KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA “MOI MARATHON”


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (kulia) akikabidhi cheti cha kutambua mchango wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kufanikisha mashindano ya Marathoni yaliyoandaliwa na Taasisi ya MOI kwa Samson Kadidi ambaye ni askari Muhifadhi Daraja la tatu TFS.

Meneja Uhusiano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Mather Chasama akizungumza kuhusu sababu za wao kushiriki kwenye mashindano hayo ya Marathoni.

Samson Kadidi (wanne kulia) ambaye ni askari Muhifadhi Daraja la tatu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS)akiwa na watumishi wengine wa Wakala huo baada ya kumalizika kwa mashindano ya Marathoni yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI)

Na:Mwandishi Wetu

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umeahidi  kuwa miongoni mwa wadhamini wataokuwa wakifanikisha mashindano ya Marathoni yanayoandaliwa na Taasisi ya Tiba na Mifupa(MOI) kwa lengo la kukusanya fedha za kuwafanyia upasuaji watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

MOI imekuwwa na utaratibu wa kuandaa Marathoni hizo kila mwaka kwa ajili ya kukusanya fedha zinazokwenda kutumika katika kusaidia matibabu yakiwemo ya upasuaji kwa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi .Katika kufanikisha mbio hizo TFS imeona kuna kila sababu ya kuwa sehemu ya wadhamini ili kuhakikisha lengo la MOI linafanikiwa.

Akizungumza ya baada ya kumalizika kwa Marathoni hiyo ambayo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alikuwa mgeni rasmi , Meneja Uhusiano wa TFS Mather Chasama ameeleza  kwa kina sababu zao wao kushiriki katika mashindano hayo ya Marathoni zilikuwa na kilometa tano, kilometa 10 pamoja na kilometa 21.

TFS imeamua kufadhili na kushiriki kwenye mashindano haya ya Marathini kwasababu inaamini watoto wadogo waliopo sasa sasa ndio wahifadhi wajao, hivyo tuliona tuna kila sababu ya kushiriki kikamilifu na tutaendelea kushirikiana na MOI kadri tunavyoweza ili kukoa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Aidha amesema kingine kilichowasukuma kuwadhamini MOI kufanikisha Marathon hiyo ni kutokana na mandhari nzuri iliyopo kwenye taasisi hiyo kwani kuna miti mingi ya vivuli na matunda, hivyo TFS inaona kuna uhifadhi mkubwa wa mazingira.

“Watu wengi wanaokuja kuona wagonjwa wao MOI na  wakati wanasubiri kuingia wodini huwa wanakaa chini ya miti iliyoko hapa, kwetu sisi tunaona MOI kama wahifadhi wenzetu, ”amesema Chasama na kusisitiza wataendelea kuguswa na mashindano yoyote yanayolenga kuisaidia jamii kuondokana na changamoto za kiafya.

Wakati huo huo ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi wote kutochoma misitu au maeneo ya hifadhi hasa katika kipindi hiki cha kiangazi ambapo maeneo mengi ya uhifadhi yamekuwa yakiathirika na moto unaotokana na baadhi ya watu kuchoma misitu.

“Napenda kutoa rai hiki ni kipindi cha kiangazi ambacho moto ni rahisi kuwaka na kuunguza misitu, hivyo wananchi wajiahadhari katika maeneo ambayo yana misitu wasitupe vipisi vya siagara au kuchoma moto kwani ni hatari kwa misitu na tukumbuke misitu ni mali, misitu ni uhai.”

Awali mgeni rasmi Waziri Ummy Mwalimu pamoja na kuelezea mikakati ya Serikali katika kukabiliana na changamoto ya watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa pamoja na mgongo wazi ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa wadau wote ambao wameguswa na kuamua kushiriki kufanikisha mashindano hayo ya Marathoni.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here