Home LOCAL TMDA YAKAMATA DAWA ZA MAMILIONI ZISIZOSAJILIWA JIJINI DAR

TMDA YAKAMATA DAWA ZA MAMILIONI ZISIZOSAJILIWA JIJINI DAR

Meneja wa TMDA, Kanda ya Mashariki Bw. Adonis Bitegeko akiwa akionesha baadhi ya Dawa zilizokutwa kwenye ghala bubu ambalo halijasajiliwa

Mmoja wa maafisa wa TMDA Kanda ya Mashariki akihakiki dawa zilizokutwa kwenye ghala bubu Dar es Salaam.


Dawa zikichukuliwa kupelekwa TMDA

Dar es Salaam.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Mashariki, imekamata vifaa tiba na  dawa ambazo hazijasajiliwa zenye thamani ya TSh 294,486,590 milioni.

Bidhaa hizo zimekamatwa kufuatia ukaguzi maalum,   uliofanyika eneo la Mtaa wa Kitumbini katika Kata ya Mchafukoge katikakati ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza eneo la  tukio, Meneja wa Kanda wa TMDA, Bw. Adonis Bitegeko amesema.

“Timu ya TMDA Kanda ya Mashariki, imefanya ukaguzi maalum katika ghala bubu kufuatia taarifa za kiinteligensia zilizofuatiliwa kwa muda mrefu.

Katika ukaguzi tuliofanya tumebaini ghala hili linalomilikiwa na mtanzania mwenye asili ya India Bw    Ramaiya Rijendra,  limehifadhi dawa mbalimbali za binadamu ambazo hazijasajiliwa kwa hiyo ubora, usalama na ufanisi wake haujulikani.

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuziondoa dawa hizo baada ya kuziorodhesha.

Ameongeza kuwa,  hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa  ikiwemo kuwatoza faini isiyopungua milioni 85 na  kuziteketeza kwa gharama zao”,

Pia tunatoa wito kwa wanaoendelea kufanya biashara hizo haramu kuacha mara moja laa sivyo  watachukuliwa hatua kali  za kisheria. Amewaonya pia wataalamu wa dawa  wanaojihusisha na biashara hizo haramu kuwa hawatosita kuwafutia leseni zao  za kitaaluma.

Aidha, amezitaja baadhi ya dawa hizo ni pamoja na; Dawa za shinikizo la damu, za kuongeza nguvu za kiume, za kutoa ujauzito na zingine nyingi.” Alisema.

“Rai yetu ni kwamba wale wote wanaofanya biashara haramu adhabu ni kali na hatutomuacha mtu”, alimalizia.

Zoezi hilo lilianza jana jioni na kufanyika usiku kucha hadi lilipokamilika asubuhi ya leo Juni 28.

Mtuhumiwa aliyekutwa nazo alipohojiwa alikiri kuendesha ghala hilo bubu pasipo na kibali na kinyume na sheria kwa kile alichodai hakufahamu taratibu zinazohusika kusajili na kuendesha biashara hiyo.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here