Home SPORTS TEMBO WARRIORS WAPEWA HESHIMA BUNGENI

TEMBO WARRIORS WAPEWA HESHIMA BUNGENI

 

Na:mwandishi wetu

Timu ya Taifa ya Walemavu ( Tembo Worriors) leo Juni 16, imekaribishwa  katika Bunge na Dkt.Tulia Akson kwa ajili ya kupongezwa na Waheshimiwa Wabunge kufuatia mashujaa hao kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini India baadae Mwaka huu.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewasilisha salamu za pongezi kwa Tembo Worriors mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Akson ndani ya Ukumbi wa Bunge leo.

Katika tukio hilo Waziri Mhe. Mohammed Mchengerwa, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na Viongozi wengine wa wizara na Timu hiyo wamehudhuria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here