Home SPORTS TEMBO WARRIORS WAFIKA POLAND SALAMA.

TEMBO WARRIORS WAFIKA POLAND SALAMA.

Na: mwandishi wetu.

Timu ya Taifa Tembo Warriors imefanikiwa kufika salama nchini Poland kushiriki mashindano ya Ulaya katika mji wa Warsaw.

Msafara huo ambao ulikuwa na wachezaji 7, Benchi la ufundi 2, Viongozi wa TAFF 2 na Viongozi wa Serikali 2 ulifika Warsaw tarehe 09 June majira saa saa moja usiku.

Kocha wa Tembo Warriors Ivo Mapunda pamoja na wachezaji wanne wanaocheza mpira wa kulipwa Uturuki wanategemewa kufika Poland leo mchana ili kufikia idadi ya watu 18 kwa msafara wa Tanzania.

Rais wa Shirikisho amewashukuru wadau wakuu wa safari hii ambao ni Wizara ya Michezo pamoja na Baraza la Michezo kwa kuwezesha ombi la TAFF kupitia benchi la ufundi lililotaka uwepo wa Michezo ya kimataifa ya kupima timu kabla ya kwenda kombe la Dunia.

“Kwakweli awamu ya Sita imefany mapinduzi makubwa katika Michezo, Na hapa ni lazima tukubali kwamba Rais Samia Suluhu amekuja na maono safi katika Michezo na tunaona matunda yake kila siku. Tunamshukuru sana kwa kuendelea kuiwezesha timu yetu hasa inapoendelea kufanya maandalizi ya kushindana Kombe la Dunia, “alisema Sarungi.

Mashindano ya Poland yanatarajiwa kuanza tarehe 11 hadi 12 Juni huku Tanzania ikipangwa kuanza mchezo wake wa kwanza dhidi ya mwenyeji Poland.
Previous articleBENKI YA DCB YASHEREHEKEA MIAKA 20 YA MAFANIKIO KWA KUTOA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WATANZANIA
Next articleWANAONYANYASA WATOTO KINGONO KUSAKWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here