Home ENTERTAINMENTS TAMASHA LA HIP HOP ASILI 2022 KUFANYIKA KWA SIKU TATU JUNI 23...

TAMASHA LA HIP HOP ASILI 2022 KUFANYIKA KWA SIKU TATU JUNI 23 HADI 25 JIJINI DAR


Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (kushoto) akifurahia jambo na Muandaaji wa Tamasha la Hip Hop Asili awamu ya pili Thomas Raymond (wa kwanza kulia) mapema leo Juni 21,2022 kabla ya kufanya mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo linalotarajia kufanyika kwa siku tatu kuanzia Juni 23 hadi 25, 2022 katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) akielezea kufanyika kwa tamasha la Hip Hop Asili linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Alliance Francaise Flora Valleur (katikati) alipokuwa akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika leo Juni 21,2022 Jijini Dar es salaam, (kushoto) ni Muandaaji wa Tamasha la Hip Hop Asili awamu ya pili Thomas Raymond.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (kushoto) akimsikiliza Mwemyekiti wa Bodi ya Alliance Francaise Mkuki Bgoya (katikati) akielezea umuhimu wa kuwepo kwa tamasha hilo.
Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Iku Kassege (kulia) pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia hotuba ya Balozi Hajlaoui (hayumo pichani) leo Juni 21,2022 Jijini Dar es Salaam.
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye mkutano huo. PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO.
 
Na: Hughes Dugilo, DAR,
Wasanii mbalimbali kutoka katika nchi za Afrika, Ulaya na Marekani wanarajiwa kuungana kwa pamoja katika tamasha la muziki wa Hip Hop Asili  awamu ya pili linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Juni 23, hadi 25,2022 katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar e s Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 21,2022 wakati wa mkutano maalum kuelezea tamasha hilo uliofanyika katika ukumbi wa alliance Francaise, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema kuwa tamasha hilo limeandaliwa kwa pamoja kati ya Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kwa kushirikiana na WePresent Tanzania kuanzia saa tano asubuhi hadi saa sita usiku.

Tamasha hili ni muendelezo wa tamasha lililofanywa na baadhi ya wana Hip Hop thelathini wa Afrika na Ufaransa Oktoba mwaka jana wakati wa Mkutano wa New Africa-France Summit (NSAF), ambao ulichocheaa kuandaliwa kwa mkakati wa ushirikiano wa Hip Hop kwa bara la Afrika kwa kipindi cha 2022/2024″ amesema Balozi Hajlaoui
 
Ameeleza kuwa tamasha hilo linaungwa mkono na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Alliance Française Dares Salaam, Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam ambapo tukio hilo la siku tatu limeandaliwa vyema kusherehekea Utamaduni wa Hip Hop Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na sanaa ya breakdancing, emceeing, graffiti, Deejaying, Beat Boxing na skate boarding.
  
Tamasha hili pia linajumuisha warsha ya siku 3 kuanzia tarehe 20 hadi 22 Juni 2022, Warsha hizo zitakuwa na maudhui kama vile Historia ya Hip Hop Tanzania, Sanaa ya Emcee, Breakdance, Beat Box .k. Wawezeshaji watakuwa Bboy Lilou kutoka ufaransa ambaye ni bingwa wa dunia wa breakdance, Deejay PH kutoka Ufaransa, Mejah Mbuya kutoka Tanzania, Mama C (Tanzania/US) na wengine”ameeleza Balozi Hajlaoui.
  
Katika tamasha hilo kutakuwa na aina mbili za tiketi, ikiwemo tiketi ya tamasha kamili na tiketi ya tamasha la Siku, ambapo gharama ya tamasha lote ni TZS 20,000/= na tamasha la siku ni TZS 10,000/=.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here