Home LOCAL SEKONDARI BUNDA YAITAKA DIT KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI

SEKONDARI BUNDA YAITAKA DIT KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI

 

Na Mwandishi Wetu, Mara
MKUU wa shule ya Sekondari Bunda iliyopo Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Charles Somba, ameitaka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuwa na muendelezo wa programu ya uhamasishaji kuhusu mtoto wa kike kupenda masomo ya Sayansi.
Somba ameyasema hayo alipokuwa anafungua programu ya kuwahamasisha mabinti iliyoratibiwa na kuongozwa na wataalam kutoka DIT iliyofanyika shuleni hapo ikihusisha shule nne za sekondari za Wilaya hiyo ambazo ni shule ya Sekondari Sazila, Rubana na Nyendo Sekondari pamoja na Bunda.

Naipongeza Taasisi hii, hiki mnachokifanya ni kitu kizuri, maana wakati mwingine tunafundisha hawa lakini wasipoona kwa uhalisia kama ambavyo mmekuja hawaweki bidii ila sasa hata ninyi mabinti mmeona wamama wanasayansi hawa hapa kazi kwenu mjitahidi,” alisema.
Aidha, Somba aliiomba DIT kupanua wigo ili kuhakikisha watoto wa kike wanahamasika hata ikiwezekana wanapoingia kidato cha kwanza ili waweze kuwajengea uelewa mapema na hii isiwe Bunda pekee, ikiwezekana fanyeni kila mkoa hata nchi nzima.
Mratibu wa program ya uhamasishaji Dk. Triphonia Ngailo alisema, kwa sasa idadi ya watoto wa kike wanaohitimu masomo ya Sayansi bado ipo chini ambapo takwimu zinaonesha wanawake wanasayansi ni 21% wakati wanaume ni asilimia 79% hivyo DIT kupitia ufadhili wa Mradi wa EASTRIP wakaanzisha programu hiyo ili wawape moyo kuwa inawezekana kwa pamoja wawatie moyo na wapambane kuhakikisha idadi inaongezeka kwa kuwa Serikali inawajali na imeweka mazingira wezeshi ili kuwapatieni ninyi elimu ili muweze kunufaika na fursa zilizopo kwenye masomo ya sayansi.
Naye Mwalimu Samora Laizer wa Bunda Sekondari amefurahishwa na program hiyo kwa kuwa inaleta uhalisia wa kile kinachofundishwa.

Hili ni jambo jema maana wakati mwingine ukifundishwa tu bila kuona uhalisia inapoteza nguvu ila kama walivyosikia leo itawaongezea nguvu” alisema Laizer
Aidha, Mwalimu Fibe Musa wa Rubana Sekondari ameishauri Taasisi kujipanga zaidi kwa kuwa jambo hilo zuri na linawasaidia zaidi hasa wanafunzi wakishahitimu masomo wanakuwa na mwanga wa kuchagua fani wanazozipenda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here