Home LOCAL RC GEITA AIPONGEZA NYANG’HWALE DC KWA HATI SAFI

RC GEITA AIPONGEZA NYANG’HWALE DC KWA HATI SAFI

 

Na. Costantine James, Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Rosemary Senyamule Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Kufuatia Kupata Hati Inayoridhisha Mfululizo kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 na 2020/21.

Aliyasema Hayo Juni 21, 2022 Wakati Akiongoza Kikao Maalumu Kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2020/21 Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Nyang’hwale.

Mhe, Senyamule ameitaka halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Kuhakikisha Inapeleka Kodi ya Zuio TRA kwa Wakati ili kuiwezesha serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Niwapongeze Nyang’hwale kwa Kuendelea Kuwa na Hati Safi, Hii Inaonesha Jitihada Zinazofanyika Katika Kukuza Uchumi wa Nchi Yetu

Ninakemea Uzembe Utokanao na Baadhi ya Watumishi wasiotambua Majukumu Yao ya Utendaji Kazi na Kusababisha Shughuli Nyingine Kukwama Kama Ucheleweshwaji wa Vifaa vya Ujenzi Lakini Pia Kusababisha Hoja kwa Uzembe” Alisema Mhe. Senyamule.

Senyamule amezitaka halmashauri zote katika mkoa wa Geita kuhakikisha zinajikita zaidi katika kutunza mazingira kwa lengo la kuweka mazingira safi na salama.

Mhe, Senyamule amewataka Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale kuhakikisha wanasema yale yote yanayotekelezwa na serikali ili Wananchi Wajue miradi mbalimbali inayotekelezwa na seriakli kataika maeneo yao.
Awali Mkaguzi Mkuu wa Nje mkoa wa Geita CPA Richson Ringo Aliwasihi Watumishi na Viongozi Kufanya Kazi kwa Kuzingatia Taratibu, Miongozo na Sheria Mbalimbali Zikiwemo za Bajeti, Fedha, Kazi, Manunuzi.

Kwa Upande Wake Bi. Sania Mwangakala Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Alisisitiza Kuwa Halmashauri Zinapaswa Kuzingatia Kuwa kwa Sasa Zinapimwa Kupitia Vigezo Vitano Ikiwemo Utekelezaji wa Hoja za CAG.

Pamoja na kujikita zaidi katika ukusanyaji wa Mapato, Upelekaji 40% ya Mapato ya Ndani Kwenye Miradi ya Maendeleo, Kutoa Mikopo ya10% ya Mapato ya Ndani kwa Kundi la Vijana, Wanawake na Wenye Ulemavu, Lakini Pia Kufuatilia Marejesho ya Mikopo Hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bw. John John Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Husna Toni Walisema Kuwa Wanaishukuru Ofisi ya Mkoa wa Geita kwa Ushirikiano mzuri.
Wamesema Wataendelea Kutoa Ushirikiano kwa Wakaguzi Ili Kuondoa Hoja Zilizosalia na Kwamba Watajitahidi Kuongeza Nguvu Kwenye Kuongeza Vyanzo vya Ukusanyaji Mapato katika Halmashauri hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here