Home LOCAL RAIS SAMIA SULUHU AMUAPISHA JENERALI JACOB JOHN MKUNDA KUWA MKUU WA MAJESHI...

RAIS SAMIA SULUHU AMUAPISHA JENERALI JACOB JOHN MKUNDA KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI (CHIEF OF DEFENSE FORCES-CDF) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Cheo kipya cha Jenerali Jacob John Mkunda kabla ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (Chief of Defense Forces-CDF) katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022. 
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Luteni Jenerali Salum Haji Othman kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff -C of S) katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali waliohudhuria tukio la Uapisho wa Mkuu wa Majeshi pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania lililofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (Chief of Defense Forces-CDF) Jenerali Jacob John Mkunda na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff -C of S) Luteni Jenerali Salum Haji Othman katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here