Home LOCAL RAIS SAMIA AKABIDHI MAGARI 224 KWA MAMLAKA ZA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA...

RAIS SAMIA AKABIDHI MAGARI 224 KWA MAMLAKA ZA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF) KWA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama wakati wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi la kukabidhi magari 224 kwa Mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Tanzania Bara na Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kukabidhi magari 224 kwa Mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Tanzania Bara na Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama wakati akitembelea kukagua sehemu ya magari 224 kabla ya kuyakabidhi kwa Mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Tanzania Bara na Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari mfano wa Ufunguo kama ishara ya kukabidhi gari kwa ajili ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Mkoa wa Njombe katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi wa Uratibu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bi. Siajabu Pandu mfano wa funguo kama ishara ya kukabidhi gari kwa ajili ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
 

 
  
Sehemu  ya Viongozi pamoja na wananchi wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akizungumza kabla ya kukabidhi magari 224 kwa Mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Tanzania Bara na Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama JijiniDar es Salaam.
  Muonekano wa Magari 224 yaliyokabidhiwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here