Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika Juni 6, 2022 kwenye Ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Bi. Fatma Khamis alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na Marekani, Uingereza, Uturuki, China, Egipty, Pakistan, Algeria, Namibia na Nigeria, na kwamba nchi hizo tayari zimethibitiaha kushiki maonesho hayo.
“Tayari nchi hizo zimethibitisha ushiriki wao kwenye Maonesho ya mwaka huu, pia ni fursa kubwa kwa wafanyabiara wetu kubadirishana uzoefu wa kibiashara na kufikia malengo yao” alisema.
Mkurugenzi huyo alIsema Katika maonesho hayo kutakua na matukio mbalimbali ya burudani ambapo katika ukumbi wa DOM uliopo ndani ya viwanja vya Julius Kambarage Nyerere kutakua na burudani na matukio mbalimbali ambayo yatakua yanafanyika kwaajili ya kuhakikisha wageni wanaotembelea maonesho hayo wanapata burudani.
Aidha aliongeza kuwa katika maonesho hayo kutakuwepo na mambo mengi mapya ambayo wameyaandaa ili kuwapa wananchi fursa ya kujifunza na kuona bidhaa tofauti kutoka kwa wafanyabiara wa hapa nchini na nje ya nchi.
“Tunategemea kuwepo na jopo la wakurugenzi wanawake katika siku hiyo ya batiki hivyo wanawake wafanyabiara wa batiki watapata fursa hiyo na kutanua wigo wa soko lao” aliongeza.
Pia alitoa wito kwa wananchi wote hususani wakazi wa Jiji la la Dar es Salaam na mikoa ya jirani kujitokeza kutembelea maonesho hayo na kwamba kutakuwa na mfumo wa kidigitali utakaosaidia kupunguza msongamano wa watu kukata tiketi na kwamba kutakuwepo na miundombinu wezeshi ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka DART kufika kwenye maonesho hayo.