Home BUSINESS NAIBU WAZIRI MASANJA AKUTANA NA UJUMBE WA BARAZA LA MADIWANI LA WILAYA...

NAIBU WAZIRI MASANJA AKUTANA NA UJUMBE WA BARAZA LA MADIWANI LA WILAYA YA USHETU

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amekutana na Ujumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu la Mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Peter Cherehani kwa lengo la kuwasilisha changamoto za ukosefu wa maeneo ya malisho katika Pori la Ushetu Ubagwe.

Kikao hicho kimefanyika leo Juni 16, 2022 katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, Swagaswaga jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Cherehani ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kutuma wataalamu kwenda jimbo la Ushetu kuwasikiliza wananchi na kuwatafutia ufumbuzi wa suala hilo.

Mhe. Masanja ameahidi kufanyia kazi mapendekezo hayo na kuhimiza kuuhifadhi msitu huo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na badae.

Pori la Ushetu Ubwage lenye ukubwa wa hekta 52,000 ni msitu wa asili ambao unamilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here