Home LOCAL MSAMAHA WA MATIBABU HUTOLEWA KWA WATU WASIO NA UWEZO – DKT. MOLLEL

MSAMAHA WA MATIBABU HUTOLEWA KWA WATU WASIO NA UWEZO – DKT. MOLLEL

Na: WAF – Bungeni, Dodoma.

Licha ya matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza kuwa na gharama kubwa na yana hitaji tiba wakati wote, Serikali imekuwa ikitoa msamaha wa matibabu kwa wagonjwa wanaougua magonjwa yasiyoambukiza ambao wamethibitika kuwa hawana uwezo wa kugharamia matibabu yao kwa mujibu wa Sera ya Afya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Chaani, Mheshimiwa Juma Usonge Hamad aliyehoji Serikali ina mpango gani wa kutoa matibabu bure kwa maradhi yasiyoambukiza kama Kisukari, Presha na Shinikizo la Damu.

Hata hivyo Dkt Mollel amesema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ambao utawezesha wananchi wote kupata huduma za afya katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.

Akijibu Swali la nyongeza lilioulizwa na Mheshimiwa Usonge aliyehoji usumbufu wanaopata wazee pindi wanapoenda hospitalini kupata huduma za matibabu, Dkt. Mollel ameendelea kuwasisitiza wataalam kufuata maagizo yanayotolewa na viongozi ikiwemo kuhakikisha Wazee wanapata matibabu bure katika vituo vya kutolea huduma za afya.

“Nitumie fursa hii kutoa agizo kwa Waganga wote wa Mikoa na Wilaya, suala la matibabu kwa wazee ni bure na wanatakiwa kuwa na dirisha lao la kupata huduma, hatutegemei kusikia tena malalamiko ya wazee wanapitia mlolongo mrefu wa kupata huduma za matibabu” amesisitiza Dkt. Mollel.

Previous articleSUSAN BUFFET FOUNDATION KUIPATIA TANZANIA DOLA MILIONI 15 KWA AJILI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI
Next articleTWCC WAFIKIENI WANAWAKE VIJIJINI: WAZIRI DKT. GWAJIMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here