Home LOCAL MRADI WA MAJI KIJIJI CHA IKINA WAKAMILIKA, WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI

MRADI WA MAJI KIJIJI CHA IKINA WAKAMILIKA, WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI


Na: Costantine James, Geita

WANANCHI wa kijiji cha Ikina kata ya Bukoli wilayanai Geita wameipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Vijijini  (RUWASA) wilaya ya  Geita kwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji katika eneo lao.

Wananchi hao wamesema kabla ya ujenzi wa mradi huo walikuwa na changamoto ya upatikanaji wa  maji safi na salama  katika kijiji chao hivyo wameipongeza Ruwasa kwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo.

Wamesema walikuwa wanatumia muda mrefu kufata maji umbali mrefu na Sasa Ruwasa imewasogezea maji katika maeneo yao.

Ruwasa wilaya ya Geita imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha ikina ambapo mpaka sasa ujenzi wa mradi huo umefikia  asilimia 98%, ujenzi wa mradi huo umehhalimu kiasi cha Milioni 120.

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Geita Mhandisi Sande Batakanwa  amesema mradi huo utahudumia wananchi 8900 katika kijiji cha ikina kata Bukoli.

Amesema kupitia mradi huo Ruwasa imejenga vituo 6 vya kuchotea maji pamoja na kujenga tanki kubwa lenye ujazo wa Lita 50,000 kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata maji kwa urahisi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here