Home LOCAL MAJALIWA APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI YA ANWANI ZA MAKAZI

MAJALIWA APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI YA ANWANI ZA MAKAZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa operesheni ya anwani za makazi kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam,

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya utekelezaji wa operesheni anwani za makazi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam,

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa operesheni anwani za makazi, Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Juni 18,2022

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIR MKUU, Kassim Majaliwa amezitaka taasisi zote zenye dhamana ya masuala ya ardhi na makazi kuhakikisha zinakuja na mikakati thabiti ya kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi iliyoainishwa wakati wa utekelezaji wa zoezi la operesheni ya anuani na makazi

Ametoa wito huo leo Jumamosi (Juni 18, 2022) wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la operesheni ya anuani na makazi, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

“Pia toeni miongozo ya namna bora ya kushughulikia changamoto za Watanzania wenzetu kuishi katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria Ili kuhakikisha wananchi wote wananufaika na fursa zitokanazo na zoezi hili”

Aidha, Waziri Mkuu amewataka viongozi katika ngazi zote hususan kwenye Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utunzaji wa mifumo sambamba na kulinda miundombinu ya anwani za makazi kwenye maeneo yao.

“Viongozi na Watendaji hakikisheni kuwa jamii inaendelea kuelimishwa ili kujua manufaa sanjari na kutumia fursa zitokanazo na uwepo wa anwani za makazi katika maeneo yao”

Pia, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara zote, Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa kuendelea kushughulikia changamoto zote zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa operesheni anwani za makazi na kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu.

“Mpango wa Uendelezaji wa Mfumo (System Sustainability Framework) unaotoa mwongozo wa shughuli zote za anwani za makazi zitakavyofanyika utumike vizuri ili kufanya zoezi hili kuwa na thamani wakati wote”

Naye, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleimani Abdulla amesema ni matarajio ya watanzania kuwa kukamilika kwa operesheni ya anuani na makazi kutasaidia kuongeza uwezekano wa kuendelea kukuza uchumi kuwa kidijitali.

kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kuwa hadi kufikia Mei 31, 2022 kupitia operesheni ya anuani na makazi taarifa na anuani za makazi 12,385,956 zilikusanywa sawa asilimia 106.94 ya lengo lililokusudiwa “hii ni zaidi ya lengo tulilojiwekea awali la kukusanya taarifa na kutoa anuani za makazi 11,582,106”.

Previous articleBRELA YAWASHIKA MKONO WATOTO YATIMA
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 19,2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here