Home SPORTS KOCHA MPYA SIMBA NI MSERBIA

KOCHA MPYA SIMBA NI MSERBIA


MWANDISHI WETU

KLABU  ya Simba imemtangaza,Zoran Manojlovic kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo akichukua mikoba ya Pablo Franco ambaye alichimbishwa Mei 31,2022.

Kocha huyo raia wa Serbia aliwahi kufundisha ndani ya kikosi cha Al Hilal ya Sudan hivyo ana uzoefu na soka la Afrika.

Ana umri wa miaka 59 hivyo anakuja Tanzania kuendeleza mipango ya timu hiyo ambayo kesho ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Mbeya Kwanza.

Ikumbukwe kwamba Pablo alifutwa kazi ndani ya  kikosi cha Simba kutokana na kushindwa kufikia malengo ambayo alipewa ikiwa ni pamoja na kutwaa taji la ligi pamoja na lile la Kombe la Shirikisho.

Mchezo wa mwisho kukaa benchi kwa Pablo ilikuwa Mei 28 alipopoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here